Text Size

KANISA KATIKA USITAWI NA MAENDELEO YA TANZANIA

KANISA KATIKA USITAWI NA MAENDELEO YA TANZANIA
RISALA Y A MAASKOFU WA TANZANIA KWA UKUMBUSHO WA MIAKA 100 YA KANISA KATOLIKI HAPA NCHINI (1868-1968)

1. MIAKA MIA YA KANISA
Kamsa Katoliki lilianza kazi yake hapa Tanzania bara miaka mia moja iliyopita, Padre Homer alipofika Bagamoyo mwezi Machi 1868. Leo Kanisa Katoliki limepata kujulikana. nalo sass lafanya kazi popote nchini. Sm sore to viungo vyenye uhai vya kanisa hili. Miaka mia moja iliyopita Kanisa h`hlkuwa kama mbcgu ndogo iliyofichika ardhini. Leo limekuwa mtu mzima, na katika matawi yake ndege waweza kuweka viota vyao.
Mwaka 1968, timataka kuadhimisha mwaka wa mia moja wa Kanisa katdca nchi yetu. Katika mwadhimisho huu, yatupasa awali ya kwanza kumshukuru Mungu, kwa manna ni Yeye aliyetenda hayo yote. "Hii ni kazi ya Mungu, nayo ni ya ajabu machoni petu. "Ni Yesu mwenyewe aiiyetuita na kutupa neema yake na ukweli wake. Kama Kanisa halijengwi na Bwana, haliwezi kusimama. Pill tunataka kuwakumbuka watu wale wote, waume kwa wake, wahosaidia kanisa lull kama tulionavyo leo: Mapadre, Mabruda, Masista na maelfu ya Wakzistu wema waliojenga Kanisa letu katdca miaka hii mia moja tangu Padre Homer mpaka sasa, wakahubiri neno la Mungu na kuwatumdcia watu wore. Tatu, kwa jina la Wakatoliki wote wa Tanzania, tunataka kujitolea terra kwa kazi bii kubwa ya ukuhani na kuwatiunikia watu - kazi tuliyoitiwa na Yesu Knstu.
2. WITO WA WAKRISTU WA KUTLTNUKIA
Imam yetu ya Kikristu ni imam ambayo hanna budi kutupa kupenda, kujitolea na kutumikia. Katika Barua ya mt. Yakubu Mtume tunasoma : "Ndugu zangu. yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imam, lakini hana matendo? Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akawaambia: Enendeni zenu kwa amam, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwiliL yafaa nini? Vivyo hivyo na imaani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake." (Yak.2, 14-17).
Yesu Kiistu mwenyewe ametuambia kwamba hakuja kutumikiwa bali kuturrukia. Ndivyo na mciistu aliye mkristu wa kweli, nalo Kanisa lataka waktistu wa kweli, sio wakristu wa jina tu. Wakristu wa kweli humfuasa Kristu. Huwatumikia wenzi wao - watu wote; nao hufanya hivyo, siyo to katika mambo ya dini, lakini huwasaidia watu walio kando yao katika mahitaji yote ya kawaida, katika furaha na matumaini yao, katika taabu na kazi zao, katika shida zao za kila siku. Daima na popote mapendo ya kikristu havana tofauti, bali yaweza kuonyeshwa kwa njia mbalimbali, kwa magna mahitaji yake ya watu ni tofauti mara kwa mara hapa na pale.
3. MAFUNDISHO YA SIKU HMI YA KANISA KATOLIKI
Basi, sisi Watanzania tulio hai mwaka huu wa 1968, yatupasa kuonyesha imani yetu ya kumfuata Yesu Kristu, na kuonyesha mapendo yetu ya kuwatumikia watu wengine, kama Injili invyofundisha dunia na kwa kadiri ya mahitaji ya jumuiya ya watu leo. Maiitaji hayo ni mahitaji gani? Tuna bahati njema kwamba Kanisa letu na Serikali yetu vimetupa maongozi mengi juu ya jambo hili. Mtaguso wa Vatikani uliokutanika toka mwaka 1962 mpaka mwaka 1965, ukahudhutiwa na Maaskofu wa Tanzania umewapa Wakristu mafundisho mengi juu ya maisha yao na wajibu wao leo. Hapa tunakumbusha hasa sala kubwa ya Mtaguso huo uitwayo "Furaha na Tumaini". Katdta sala hiyo Mtaguso umekuwa kazi ya wakristu duniani leo.
Tena mwaka jana Baba Mtakatifu Paulo VI ameandika Barua mbili muhimu juu ya mahitaji ya jumuiya za watu leo. Barua va kwanza iitwayo "Ustawi wa Walimwengu" inaomba Kanisa na watu wote wenye mapenzi mema wazisaidie kwa jtunla nchi zinazoetidelea. Barua ya pili ni tisala maalum kwa Wakuu wa Kanisa na kwa watu wa Afika. Tunashukuru kupata iisala hizi mbili kwa sababu zatuonvesha maisha yao, nasi tunatumami idadi kubwa venu mtazisoma kwa makini.
4. AZIMIO LA ARUSHA
Wakati huo huo hapa Tanzania Rais wetu na TANLU wametoa hati ya tatu muhimu ya kutuongoza katika maisha yetu. Had hiyo ni Azimio la Arusha. Hakuna aliye na shaka kwamba katika Azimio la A usha yamo mafundisho mengi tunavohitaji mno sisi kwa maendeleo na heri va jumuiya yetu leo. Hakuna aiiye na shaka kwamba katlka Azimio la Arusha tunaweza kupata mafundisho ya kweh ya kufaa maisha ya binadamu na jumuiya ya watu. Mafundisho havo yamesisitizwa kwa narnna ya kutumiwa leo na watu wa Tanzania. Tunaweza kuona pia jinsi hilo Azimio la Arusha linavyopatana na roho ya kweli ya Knstu na Kanisa, roho ya udugu, roho ya kushitikiana, kutumnilcia na kufanya kazi kwa bidii.
Tunapolifikiria Ammo la Arusha, yatupasa kukumbuka pia de bidii ya wakristu wa mwanzoni, iiivyoandikwa katika matendo ya Mitume: "Jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; ball walikuwa na vita vyote shirika Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji. (Mdo. 4, 32, 31). Tunaomba myawaze mambo hayo kama Mt. Pauli alivyotushauri: "Mvue kwa habaii ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenve kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya .... mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa manna to viungo, kiln mmoja kiungo cha mwenzake". (Efe. 4, 22, 23-25).
5. CHEO CHA MWANADAMU:
Kila Seiikali njema ya watu, msingt wake unapasa kuwa kuheshimu cheo cha mwanadamu. Tunafurahi sana kwamba, tena na tena, tangu nchi hii kuwa huru, na tena katika Ammo la Arusha, viongozi wa Serikali yetu wamesisitiza msingi huu wa heshima iliyo halo ya kila mtu pasipo kujali taifa lake, elimu yake, na utajiri wake. Watu wote ni sawn, na kila mmoja binafsi ana haki na cheo chake na heshima yake. Basi haikubaliki kwamba warn wengine, kwa kuwa to wamechelewa kupata maendeleo ya uchumi na ufundi wa dunia ya kisasa, wataendelea "kugandamizwa, kupokonywa na kudharauliwa". (AD p.4).
Sasa Azimio la Arusha laonyesha nia ya Serikali ya kutaka kuleta cheo cha binadamu kwa matendo katika matumizi ya kila siku yc uchumi. Nia yenyewe ni kuwapa watu wote wa taifa hili nafasi iliyo ya haki ya kuendelea kila mtu nchini, ill mtu ycyote au kikundi chochote cha watu wasiweze kuwapokonya wenzao kwa njia yoyote ile. Serikali inataka hasa kulinda haki za wale wasioweza kujitetea, yaani baadhi kubwa ya Watanzania ambao hawakupata elimu ya sekondari, wanaoishi mashambani. Ni wajibu wa Serikali na Kanisa kulinda kaki za wale wasiokuwa na riziki za dunia hii. Ndiyo magna Kanisa limefurahi kwamba Serikali imedhihiiisha kwa nguvu nia yake ya kutaka kuona kuwa mapato va Tanzania yatati miwa kwa busara, "kwa manufaa ya taifa ama, wala si kwa manufaa ya mtu mmoja au watu wachache tu. (AD.p17). Kwa hiyo taifa zima la Tanzania litaweza kusonga mbele pamoja kutoka katika hall ya umaskini na kuingia kat ka hail ya ustawi. (AD.p 11).
6. UJAMAA, UHURU NA KUJITEGEMEA
Katika kazi hii kubwa ya kuisitawisha nchi kwa njia ya amani, zaidi ya cheo cha binadamu tunataka kuwakumbusha mambo mengine matatu yanayotokana na cheo hicho. Mambo hayo ni ya msingi kwa Azimio la Arusha na kwa maisha ya kweli ya kikiistu. Jambo la kwanza m ujamaa wa watu, yaani ile roho ya udugu inayoonekana katika kushhikiana na kutiunikia. Jambo la pili m uhuru, upaji mkubwa wa Mungu kwa kila mtu. Uhuru humfanya kila mmoja wetu afahamu na kuamini kwamba yeye si kiwnbe cha kuhmuzwa wala kutumiwa kama mtumwa. Jambo la tatu m juhudi ya kufanya kazL Waume kwa wake wafanye kila wawezalo kwa manufaa yao wenyewe na manufaa va watu wengine. H iyo ndiyo roho ya kujitegemea, ambayo siku zote ni tabia ya jamii yenye nguvu, jumuiya yenye nguvu, na Kanisa lenye nguvu.
7. MAPOKEO YA TANZANIA.
Hoja hizi ni kwa watu wote. Lakini kale kuzitumia hapa na leo kwataka kulingane na mapokeo yetu, utamaduni wetu, na mahitaji yetu wenyewe. Sisi huku Tanzania twapaswa kujifunza mengi kutoka kwa watu wengine na nchi nyingine kwa maana Tanzania ni sehemu ya duma moja na Watanzania m sehemu ya taifa moja la binadamu, na sisi sote m viungo vya Kanisa Katoliki la dunia nznna. Uhuru usiwe na magna ya kujitenga. Lakini pia tusiige kitumwa watu wengine. Watanzania wana kila haki ya kujionea fahari na nchi yao, mapokeo yao ya tangu kale na historia yao ya siku hizi. Leo wao, sawa kama watu wengine, yawapasa kutafuta namna ya kuishi na namna ya Serikali inayoafikiana na hali vao wenyewe. Maanfa mbalimbali ya tangu zamani ya kila taifa, na utamaduni wa ama nyingi, ni msaada mkubwa wa kukuza maarifa ya watu, nasi yatupasa tujue kushiril ishana maarifa hayo.
8. WATU NDIO MSINGI WA MAENDELEO
Huku Tanzania upo msingi wa kweli wa maendeleo thabiti, nao watu wenyewe ndio msingi. Maendeleo ya kweli ni lazima yategemezwe na tabia yao njema, ushujaa wao, na nia yao njema. Yategemezwe na uhora wa hekima zao za jadi na utamaduni wao, na imam zao za dini. Yategemezwe na nia yao va kujifunza mambo mapya, na roho ya kushirikiana, na husara yao ya umoja, na jasho lao wenyewe. Na hayo vote kwa ajili ya kusaidiana.
9. UJAMAA
Waafrika wanafahamu maana ya mapendo ya kidugu, kuliko watu wa baadhi nyingine nyingi za dunia ya leo. Kwa vizazi vingi watu wameishi maisha ya udugu katika jamaa kubwa, katika koo zao na katika vikundi vya kikahila. Hali hii thabiti ya ujamaa, pamoja na maarifa yake mengi ya kushirikiana katika hali zote 7a maisha, si kitu kigeni. Ni kinyume chen_yewe cha kujipendelea nafsi na fikira za uhinafsi, ambavyo hasa ni vigeni kwa tabia za kiafrika. Kwa hivo si ajahu kwamha maendeleo ya uchunu wa 'I Tanzania yatakuwa na msingi wake imara katika fikira mpya za udugu wa kiafrika na ushikamano wa jamaa: "Ujamaa"