Text Size

Kwa Waamini na Watu Wote Wenye Mapenzi Mema

Kwa Waamini na Watu Wote Wenye Mapenzi Mema
Mwaliko wa Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2000: Tutafute Faida ya Wote
15 june 2000

1. UTANGULIZI
Wako watu wanaojiuliza, "Je, ni kwa nini Kanisa linajishughulisha na uchaguzi wa kisiasa?" Kama waamini Mungu anatualika kutakatifuza ulimwengu iii kujenga Ufalme wake. Ufalme huu unajengwa hapa duniani kwa njia ya kudhihirisha upendo katika mipango ya kibinadamu. Kwa hiyo ni wajibu na haki ya Kanisa na mashirika ya dini zote kuchunguza, kuchambua, kuelimisha na kutetea juu ya haki za kibinadamu na haki za watu, iii utu wetu uwe msingi wa sera zetu - kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Sisi Maaskofu Katoliki Tanzania tunataka kushiriki katika wajibu hub. Nia yetu ni kwamba tuwe na uchaguzi mkuu wa amani na haki unaolenga katika kujenga nchi yetu kwa kuzingatia maendeleo na faida ya wote.
2. MAANDA LIZI NA UTARATIBU WA UCHAGUZI
2.1. Tume ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo mhusika mkuu katika kusimamia utaratibu wa uchaguzi. Tume ihakikishe kwamba taratibu na maelekezo ya uchaguzi yanakuwa wazi na uchaguzi wenyewe unakuwa huru, wa haki na amani. Aidha, Tume ihakikishe kuwa vyama vya siasa, wagombea na wananchi wote wanaelewa vizuri utaratibu wote. Maelezo yawe kamili, sahihi na yatolewe kwa wakati muafaka iii kuondoa wasiwasi juu ya taratibu zote za uchaguzi huo.
Jamii ya kiraia na watu wote washiriki kutafuta maelezo toka Tume na kuhakikisha kuwa mambo yanafanyika kulingana na taratibu. Jamii inao wajibu kusaidia Tume kutekeleza wajibu huo wa kidemokrasia kwa kutoa taarifa wakati wote.inapohitajika.
2.2. Vyama na Wagombea
Wapiga kura wanayo haki ya kujua sera za vyama mbalimbali na mikakati watakayotumia wagombea kutekeleza sera hizo. Vilevile wananchi wajue jinsi wagombea wanavyoteuliwa na vyama vyao. Kuwa mgombea ni wito wa kuwa mtumishi wa watu. Tunatoa shukrani za pekee kwa wale ambao wana moyo wa kugombea kwa lengo la kutumikia. Taifa letu litajengwa na watu wa namna hiyo wanaosukumwa na dhamiri safi na kujitoa mhanga, kama Maandiko Matakatifu yanavyosema: "Mimi ni Mchungaji mwema. Mchungaji mwema huyatoa maisha yake kwa ajill ya kondoo wake. Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa.sababu yeye ni mtu wa mshahara tu" (Yn 10:11¬13).
Jamii ina haki ya kupata viongozi wanaostahili na wanaofaa. Ni wajibu na haki ya jamii kutafuta maelezo juu ya sera na mikakati ya vyama. Wagombea waeleze sera hizo kwa uaminifu na uadilifu. Jamii ielewe kuwa ipo tofauti kati ya ahadi na utekelezaji. Pia wagombea wajue kwamba kutoa ahadi hadharani ni kama deni.
2.3. Jamii za Kiraia na Wapiga Kura
Sisi Watanzania tumo katika makundi mbalimbali ya kiraia kadiri ya shughuli zetu kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wafanyabiashara, mashirika yasiyo ya kiserikali, n.k.
Jamii hizo za kiraia zinaalikwa. kuendelea kuwatia moyo wananchi wenye sifa na moyo wa kujituma kugombea uongozi katika ngazi zote. Pia jamii zijifunze na zijishughulishe kujenga umoja na mshikamano katika kutetea haki na mahitaji ya wote katika Majimbo ya Uchaguzi na katika Taifa. Mashirika ya dini na jamii za kiraia zishiriki kuhamasisha watu juu ya uchaguzi mkuu bila kujiingiza katika kampeni za vyama vya siasa. Watu waelimishwe kuwa kura yao ya kuchagua viongozi hainunuliwi na vichocheo kama vile kanga, "T-shirt", fedha, n.k.
Ili kutimiza haki hii ni wajibu na mwito wa Mungu kwa kila raia mwenye umri wa kupiga kura kujiandikisha na kupiga kura.
3. HITIMISHO
Tunawahimiza waamini na watu wote wenye mapenzi mema, muuone uchaguzi huu kama wajibu utokao kwa Mungu. Ushiriki wetu katika makundi mbalimbali utokane na msukumo wa ndani wa kutaka kujenga Taifa letu kuwa mahali pazuri zaidi pa kuishi kwa pamoja. Tujifunze kutokana na historia na uzoefu wetu katika ujenzi wa demokrasia shirikishi, kuchagua viongozi wenye mwelekeo sahihi wa Taifa letu. Kristo anatufundisha katika Maandiko Matakatifu: "Mimi nimekuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yn.10.10). Kudumisha na kuendeleza uzima huu ni wajibu wetu. Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
+ Justin T. Samba
RAIS
BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA