Text Size

Press Release

Press Release
9 Juni 2000

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference - TEC), lenye idadi ya Maaskofu 29, Juni 7, 2000 lilianza vikao vyake, ikiwa ni pamoja na kikao cha 35 cha Kamati Tendaji (Permanent Council) na mkutano mkuu wa 53 wa mwaka kwenye Kituo chake cha Mikutano na Mafunzo - Kurasini Centre chini ya Rais wake,.. .Mhashamu Askofu Justin Samba wa Jimbo la Musoma.
Pamoja na ajenda nyingine, vikao hivi vitakuwa na kazi ya kupitisha bajeti ya Secretariat ya TEC, kujadili mipango ya Baraza kwa kipmdi cha miaka 2000 - 2003 na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi yake mbali mbali ya hapo awali.
Aidha vikao hivi vitajadili pia mfuko wa ushirikiano baina ya Caritas Australia na Shirika la misaada la Caritas Tanzania ambao pamoja na mambo mengine utasaidia uhakika wa chakula na lishe, miradi ya maji, Wakimbizi na akina MAMA, WATOTO na VIJANA:
Juni 12 Mkutano utazindua Katekisimu ya Kanisa Katoliki ambayo ni kanuni ya mafundisho ya imam ya Kanisa Katoliki. Aidha siku hiyo hiyo kitazinduliwa pia kitabu cha Ibada ya Sakramenti ya Ndoa.
Mengine yaliyomo katika ajenda ni taarifa ya kusajiliwa kwa Chuo Kikuu Katoliki cha Mt. Augustine (SAUT) cha Nyegezi, Mwanza kuwa Chuo Kikuu kamili na tuarifa juu ya katua za maendeleo ya vyuo vyake vishikiki Bugando, Mwanza; Mwenge, Moshi; na Songea. Maadhimisho ya Jubilei Kuu 200; Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000; Maandalizi ya Mkutano wa Umoja Mabaraza ya Maaskofu Katoliki wa Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) na Katiba ya Tume ya Maisha ya Wakfu. Umoja huo wa mabaraza ulizaliwa Dar es Salaam mwaka 1961. Mwaka huu pia Baraza litachagua viongozi watendaji wakiwemo Rais na Makamu wake watakaoongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
R. Raphael R. Kilumanga
TEC Press Secretary