Text Size

Tahadhari juu ya "Udini Mkali na Potofu" KatikaKanisa Katoliki Tanzanzia

Tahadhari juu ya "Udini Mkali na Potofu" KatikaKanisa Katoliki Tanzanzia
28 Mei 1999

I . Tunapojiandaa kuingia karne ya 21 na kuisherehekea Yubilei Kuu mwaka 2000, Kanisa Katoliki nchini mwetu linashuhudia kero na fujo zinazosababishwa na vikundi vinayoibuka ndani ya Kanisa. Vikundi hivi vina asili zake ndani na nje ya taifa letu. Ingawa baadhi ya vikundi hivi vina mwelekeo wa kikarismatika na vinaweza kuwa vimepewa ruhusa na Kanisa, tunasisitiza kuwa lazima viwe na utii na kufuata miongozo ya Kanisa mahalia. Kkkundi kinachotenda lolote kwa jina la Kanisa, ni lazima kianzishwe kwa ruhusa ya Wakuu wa Kanisa wenye mamlaka, na budi kifanye shughuli zake chini ya uangalizi na usimamizi wa Wakuu hao (Kan. 312, 315, 323, 301:1, 305#1-2). Ili kuendesha shughuli zake katika jimbo, lazima vikundi hivi vipate ruhusa ya Askofu mhusika. Ni wajibu wa Askofu kuhakikisha kuwa mambo yasiyofaa hayajiingizi katika nidhamu ya Kanisa. Hii ni kuhusiana na huduma ya Neno la Mungu, maadhimisho ya Sakramenti na visakramenti, ibada ya Neno la Mungu, heshima kwa watakatifu na usimamizi wa mali (Kan.392). Ushuhuda wetu ni pamoja na kudumu imara katika msingi na miongozo ya Kanisa Katoliki.
2. Kwa namna ya pekee, sisi Maaskofu tukiwa wadhamini wa imam na wa maadili ya Kikatoliki hapa nchini, tunapenda kukemea na kuwapa msimamo wetu kuhusu tatizo sugu la kikundi cha "Wanamaombi". Mnamo mwaka 1985, Maaskofu Katoliki baada ya kupata malalamiko juu ya uendeshaji wa "ibada" za Padre Felician Nkwera katika majimbo kadhaa kama vile Majimbo lMIakuu ya Tabora na Dar es Salaam, walimkataza asiendelee na shughuli hizo. Kwa sababu ya kukaidi na kukataa kumtii Askofu wake, alisimamishwa kutoa huduma za kipadre mnamo mwaka 1989. Hata hivyo, Padre Nkwera alishupaa na kukaidi uamuzi wa Askofu wake na kupuuza masharti aliyowekewa na viongozi wake, akaendelea na ibada zake na mafundisho yake potofu. Kadiri ya sheria ya Kanisa, hakuna mtu anayeweza kuwinga mashetani kihalali bila ruhusa rasmi na wazi kutoka kwa mkuu wa Kanisa mahalia mwenye mamlaka. Ruhusa hii hutolewa to kwa padre ambaye ana sifa za uchaji, elimu, busara, na unyofu wa moyo (Kan. 1172).
3. Sababu za msingi zinazotufanya Maaskofu tusimamishe huduma za Padre Nkwera ni kama ifuatavyo miongoni mwa nyinginezo:
(a) Tabia na mwelekeo wa maadili yake binafsi kama padre hayakuwa, na yanaendelea kutokuwa mfano bora.
(b) Kuidharau, kuidhalilisha na kuikufuru Sakramenti Takatifu ya Ekaristi kwa kuitumia kishirikina. Mtu anayetupa Sakramenti Takatifu ya Ekaristi au anayeichukua au kuiweka kwa makusudi ya kufuru, anatengwa na Kanisa moja kwa moja kutokana na sheria yenyewe. Na adhabu kama hii, huondolewa to na Baba Mtakatifu (Kan. 1367, 1376).
(c) Kusababisha mafarakano na utengano katika familia za watu wa ndoa.
(d) Kutoa na kueneza mafundisho potofu na kukashifu viongozi wa dini Katoliki wakiwemo Baba Mtakatifu na Maaskofu kiasi cha kudiriki kuwaita maruhani [free masons] (Kan.1373).
(e) Kuthubutu kuchonganisha na kufitinisha viongozi wa dini na serikali.
(f) Kuleta vurugu na fujo wakati wa ibada.
4. Kwa muda mrefu, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limevumilia likichunguza uasi na kero zinazosababishwa na "Wanamaombi". Tumaini letu lilikuwa kwamba Padre Nkwera angejirudi yeye na wafuasi wake na kurudi katika kundi moja chini ya Mchungaji mmoja. Badala yake kikundi hiki kinazidi kuleta fujo na kusababisha mafarakano katika Kanisa letu hapa nchini.
5. Tukiwa wadhamini wa imam na maadili ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, tunawatangazia waamini wote na watu wote wenye mapenzi mema kwamba:
a) Pamoja na mwelekeo wake potofu wa kimaisha, anayofundisha na kufanya Padre Nkwera ni kinyume cha miongozo ya Kanisa Katoliki. Kwa mfano, anadai kwamba nguzo mbili za Kanisa Katoliki ni kuabudu Ekaristi Takatifu na heshima kwa Bikira Maria tu. Mafundisho haya ni uzushi (heresy) kwa sababu Mtaguso wa Pili wa Vatikano unafundisha kwamba nguzo za Kanisa Katoliki ni Ekaristi Takatifu na Neno la Mungu (P0, n. 4-6; Kan. 751). Heshima kwa Bikira Maria inatuelekeza kwenye nguzo hizi mbili lakini kamwe haichukui nafasi yake.
Kwa uzushi wake, Padre Nkwera ametengwa na Kanisa moja kwa moja kutokana na sheria yenyewe (Kan.1364). Na tena, adhabu hii inaongezewa uzito kutokana na ukweli kwamba alionywa na kukatazwa na Baraza la Maaskofu Katoliki na kusimamishwa na Askofu wake na bado akaendelea kushupaa (Kan. 1371).
b) Wale wote wanaofuata, na watakaoendelea kufuata miongozo na maagizo ya Padre Nkwera baada ya tamko hili, nao watakuwa wamejitenga na kutengwa na Kanisa Katoliki. Hivyo, "Wanamaombi" popote wanapokuwa katika jimbo lolote, wanahusika na kujumuishwa katika adhabu hii (Kan. 1371, 1399).
Kwa hiyo, Padre Nkwera pamoja na wafuasi wake wote hawaruhusiwi kushiriki ibada na sakramenti, kujiunga na vyama vya kitume, wala kupata huduma nyingine za Kanisa Katoliki hadi hapo watakapobadili msimamo wao na kujieleza wazi kwa uongozi wa Kanisa pamoja na kufanya malipizi yote yanayotakiwa. Kinyume cha hayo ni kuleta fujo na uchokozi wa makusudi.
7. Tunawatakia waamini na watu wote wenye mapenzi mema heri na baraka. Roho Mtakatifu awaimarishe, msome vizuri alama za nyakati na msiyumbishwe na manabii apotofu (1Yoh. 4:1-3). Imarisheni mshikamano wenu na kuambatana daima na Bwana Wetu Yesu Kristo aliye daima Mchungaji Mwema (Yoh. 10:11).
Wenu Katika Krigto
+ Justin Samba