Text Size

Maeneleo ya Kweli ya Mwanadamu

Maeneleo ya Kweli ya Mwanadamu
Barau ya Kichungaji: Baraza la maaskofu Katoliki Tanzania
7 June 1992

 

 
 
Wapendwa Waamini
Na Watu wote wenye mapenzi mema,
BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE NANYI.
UTANGULIZI
1. Siku zote Kanisa linaguswa na jitihada za kumwendeleza mwanadamu kwa misingi inayozingatia hali nzima ya mtu na jamii anamoishi. Kwa mfano Baba Watakatifu wengi wa nyakati zetu wanatoa miongozo kuhusu nyanja mbalimbali za jamii, kama vile wafanyakazi, maendeleo ya watu, familia n.k.[1]. Ingawa Kanisa halina majibu ya kiteknolojia, linayo hekima ya kuchangia katika masuala yanayomhusu mwanadamu nyakati zote. Linafanya hivyo kwa kuutafakari Ufunuo wa Mungu na kuchota kwenye hekima yake ya karne nyingi za kulea na kufundisha. Barua hii inachukua mwelekeo huo.
Lengo letu ni kuangalia kwa mapana maendeleo thabiti ya jamii yetu ya Tanzania. Kiini au dhamira ya barua hii ni kuamsha dhamiri ya mtu binafsi na dhamiri ya jamii ili kutuwezesha kutaka na kuchagua ni yapi yanatufaa na yapi hayatufai Huko ndiko kukomaa kiutu na kijamii. Tunawaandikieni siyo to ninyi Waamini Wakatoliki, bali watu wote wanaomwamini Mungu na raia wote wenye mapenzi mema.
Sehemu ya Kwanza:MAENDELEO YA KWELI YA MWANADAMU
Nafasi ya Kanisa
Kanisa halina majibu yote ya kiteknolojia kuhusu masuala ya maendeleo kamili ya watu; wala halipendelei mfumo fulani wa kisiasa na uchumi kuliko mwingine. Linachotaka ni kupewa nafasi ya uhuru wa kutimiza ujumbe wake, nayo heshima ya mwanadamu ilindwe ipasavyo.[2] Hata hivyo Kanisa linajihusisha na wanadamu wote kikamilifu. Kwa ajili hiyo shughuli take za kiroho mara nyingi zinaambatana na juhudi za mwanadamu kujipatia mahitaji ya maisha ya furaha hapa duniani. Kusema kweli maendeleo yamfaayo mwanadamu kuendana na hadhi yake hayawezi kupatikana kwa njia za teknolojia peke yake kwani umbile la mwanadamu halieleweki pasipo kuchota elimu nje ya teknolojia. Ndiyo maana Kanisa linao mchango wake mintaarafu misingi, malengo, masharti na mengineyo kuhusu raendeleo halisi yenye uthabiti. Linapofanya hivyo linatimiza wajibu wake wa kutangaza ukweli juu ya Mungu na mwanadamu na kupambanisha mazingira yaliyopo na ukweli huo.
Nia yetu sisi Maaskofu ya kuwaandikia barua hii ni kuchangia katika kudumisha na kuendeleza maendeleo bora yenye fungamano kwa taifa zima. Tunatafuta njia itakayositawisha amani na uelewano kati ya watu wote. `funapenda kuwahakikishia.wa,Mini wetu na watu wote wenye mapenzi mema kuwa tunaguswa na kila hali ya maisha ya taifa letu, ndiyo maana tunawapatieni mtazamo wa Kanisa Katoliki.
3. Kanisa linayo Habari njema katika furaha na magumu ya Mtanzania; katika majonzi na majaribu yake; kadhalika katika matumaini na wasiwasi wake. Sisi tulio washiriki wa Kanisa lenye safari ngumu hatuna budi kusonga mbele tukiungana na wenzetu, tukiamini kuwa "Imani huleta mwangaza kwa vitu vyote; hutambulisha utimilifu kamili uliotayarishwa na Mungu kwa watu wote.”[3]
Ingawa utimilifu kamili wa maisha hupatikana katika urlimwengu ujao, hata hivyo binadamu anasukumwa kuyakabili matatizo na mabadiliko ya kila siku kwa moyo mkuu kama Mtakatifu Paulo anavyotuambia:
Basi simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda. kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya Amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Zaidi ya hayo, Imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto wa yule mwovu".[4]
MAENDELEO YA KWELI HUTEGEMEA UTII KWA MUNGU
4. Jamii yoyote inapojitahidi kujiwekea mipango na harakati za kuleta maendeleo ya kweli inahitaji iweke maanani kipengele cha kipekee kinachomwainisha mwanadamu tofauti na viumbe vingine, yaani, "aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu".[5] Mwanadamu ni umbile la "mwili na roho" vinavyoelezwa kwa ishara mbili tofauti: "Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi", na "akampulizia puani pumzi ya uhai". Mtu akawa nafsi hai.[6] Kwa kuumbwa vile mwanadamu anakuwa na mvutano na viumbe vingine duniani; na papo hapo anapewa uwezo wa kuvitawala na kuvitumia. Ndivyo alivyowekwa katika bustani awe na wajibu wa kuilima na kuitunza, avitawale viumbe vingine.[7] Ataweza haya yote kwa sharti kwamba naye ainame chini ya uwezo wa Mungu, amtii Mungu ambaye amemwekea mipaka ya kuvitawala viumbe vilivyo chini yake.
5. Kufuatana na fundisho hili mwanadamu hawezi kupata maendeleo ya kweli kutokana na mipango au hamakati zinazopuuzia misingi ya umbile lake, ikiwa nia yake ni kuvitumia vitu jinsi anavyojiamulia kiholela. Kutawala vitu na kuvitumia kwapasa kutekelezwa kwa kutii ule utaratibu mwanadamu aliowekewa na Mungu, ndiyo kusema kulingana na ile sura ya Mungu iliyo ndani yake ambayo ndiyo utukufu na shina la uwezo wake. Kwa vingine mwanadamu asipomtii Mungu na kufuata taratibu alizoziweka nayo maumbile,mengine yanakataa kumtii; yanamwasi na kumzushia dhiki na maumivu. Na siyo yeye tu, bali ria jamii nzima inaathirika.
Ukweli huu ni msingi unaodai kuzingatiwa tunapofanya mipango ya kuboresha maisha ya watu kwa kutumia utaalamu wa sayansi au teknolojia yoyote ile. Mipango yetu isipozingatia kimsingi umbile la mwanadamu la kumwelekea Mungu daima, tutajikuta tunamwangamiza mwanadamu huyo hayo badala ya kumjenga na kumwongezea furaha.[8]
6. Kwetu sisi waumini Wakristu, Yesu Kristu aliyekufa na amefufuka, ambaye ni "Mwanzo na Mwisho",[9] ndiye chimbuko la maendeleo ya mwanadamu. Yeye ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote, navyo vitu vyote viliumbwa kwake. Kwa hakika vitu vyote hushikamana ndani yake; amevipatanisha vitu vyote na nafsi yake.[10] Huu ndio mpango aliouweka Mungu tangu awali. Tunaupokea mpango huu na kuuishi kwa imani tangu tulipo hapa duniani.
Wakati huo huo tunatambua kuwa dhambi ambayo inatusonga na kulemaza maendeleo yetu imeshindwa na Mkombozi aliyetupatanisha na Mungu. Kwa nguvu yake tunaendelea kupambana na kila uovu tukitazamia ushindi mwishoni.
7. Kwa mwumini "ndoto ya maendeleo makamilifu" inaonekana chini ya mwanga wa imani; tena inawezekana to kwa sababu Mungu Baba ameamua tangu mwanzo wa ulimwengu kumshirikisha mwanadamu utukufu wake kwa njia ya Yesu Kristu aliyefufuka katika wafu. Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa wakati tungali tunapambana na vikwazo vyote vya maendeleo, siku moja "yote yatakuwa mapya",[11] mwili huu wenye kuharibika utavalishwa hali ya kutoharibika; mwili uwezao kufa utavalishwa half ya kutokufa.[12] Ndipo Bwana atautoa Ufalme kwa Mungu Baba,[13] nazo kazi na matendo yanayomstahili mwanadamu yatakombolewa. Huu ndio utimilifu wa maendeleo.
Ndiyo maana Kanisa linajisikia kuwa masuala ya maendeleo ya watu ni sehemu ya wajibu wake wa kichungaji. Kwa hiyo tunawahimiza waamini wote wajitoe kwa moyo wa kuupokea mwito huu. Kwa kweli mwito wa kushughulikia maendeleo ya watu unamhusu kila raia mwanamume na mwanamke. Aidha unahusu kila jumuiya na kila taifa. Wote wanaalikwa washirikiane kwa nia moja. Unalihusu Kanisa Katoliki na makanisa mengine ya Kikristu pasipo kusahau rnadhehebu mengine. Kanisa Katoliki liko tayari kabisa kushirikiana nayo
katika huduma hizi.[14]
8. Tunapofikiria maendeleo kamili ya mwanadamu hatuna budi kujihusisha
na maadili ya dhamiri kwa sababu matendo ya kimaendeleo yanayotegemea uamuzi wa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu. Msingi utakaotumika katika kuamua ni kufuata ile kanuni ya kuchagua kilicho chema daima. Kwa hiyo uamuzi wa kidhamiri unahusika na vitendo vyote vya maendeleo.
Hali kadhalika vyombo vya kisayansi na teknolojia pamoja na matumizi yake vinategemea uamuzi wa dhamiri kwa kupima uhalali au uhalifu, wema au ubaya unaotokana navyo. Kwa Wakristu na waamini wengine uamuzi wao utaegemea imani ya Kikristu waliyoikubali na mwanga wa neema ya Mungu.[15]
Inapotokea kwamba mipango fulani inayopotosha jamii inazuka, chanzo chake kinabakia ni uamuzi wa mtu au wanakikundi wanaohusika na mipango hiyo. Watawajibika kwa kusababisha baraka au maafa; yakini wao ndio watasababisha upotofu katika jamii wanaposimika mazingira yanayopotosha. Kadiri hatua zao zinavyoimarika na kupanuka kadiri hiyo upotofu utaenea.
9. Haturidhiki tunapochambua half ya maendeleo tusipogusia mizizi ya maovu katika ulimwengu wetu. Mara nyingi tunasema kuwa kosa limesa¬babishwa na ubinafsi, uzembe, bahati mbaya, n.k. Lakini kimya kimya inaeleweka kuna mtu hakutimiza wajibu - amekosa maadili katika dhamiri yake. Nguvu ya ukweli huu unatuchoma zaidi ndani ya moyo ikiwa tumesimika maisha yetu katika imani kwa Mungu na amri yake inatuamuru kutenda mema na kuacha mabaya. Mungu aliye mwingi wa huruma anataka tuwe watu wanaoongozwa na dhamiri safi inayotofa¬utisha jema na baya. Ni wajibu wa kila mwanadamu kusikiliza mlio huo na kuufuata. Tusipofanya hivyo tunakosa raha kwani tunajua tunamchukiza Mungu na kumwumiza jirani.[16]
Mipango inayopingana na utaratibu wa Mungu na manufaa ya jirani inaweza ikawa inaegemezwa na Falsafa mbili zenye kasoro. Moja ni tamaa ya kupata faida haramu; ya pili ni kiu ya Kutawala na Kukandamiza wengine. Mara nyingi fikra hizi hufanya kazi pamoja katika ulimwengu wa leo. Wanaosukumwa na fikra hizi siyo to watu binafsi Bali yanaweza yakawemo mataifa au hata shirikisho la Kimataifa.
Kwa kujivalia ngozi ya maendeleo ya watu wanasimika mizizi inayoharibu maadili bila watu wenyewe kufahamu. Fikra hizi zinaweza pia kuehochea mipango ya kiuchumi ama ufadhili kumbe kwa yakini ni vyombo vinavyotumikia miungu fulani: fedha, itikadi fulani, au teknolojia.
Lengo letu la kuchambua mawazo haya ni kuonyesha kuwa maendeleo kamili ni jambo la kuamua kidhamiri yaani kuchagua lililo jema na kukataa lililo baya. Jamii inayokubali kuendeshwa na fedha, itikadi au teknolojia kama ndiyo miungu yenye neno la mwisho katika maisha ya wana jamii inajijengea maadui wa kuibomoa yenyewe.
10. Tumalizie sehemu hii kwa maamuzi mawili muhimu: Mosi, tunapofikiria maendeleo ya jamii ni haki yetu kujichagulia na kujiamulia aina ya maendeleo tunayotaka kuendana na heshima ya tunu zetu za kiroho, za Kimaadili, za Kiimani, na Kiutamaduni[17] ambazo ni nguzo za heshima ya binadamu na uzalendo wa taifa letu. Bila tunu hizi, upatikanaji wa mali, wa vitu vya teknolojia, hata kunyanyuka kwa pato la kila mtu, hautaleta maendeleo yanayomstahili mwanadamu. Pili, yeyote anayppenda kuwa mfadhili wetu aelekezwe akubali kuheshimu'tunu tunazozithamini sisi wenyewe.
MMOMONYOKO WA MAADILI KATIKA JAMII
Katika kuimarisha uzalendo wetu, yakiwemo maingilio na tamaduni, uchumi, na fikra za mataifa mengine, kumetokea utepetevu wa maadili katika nyanja mbalimbali, hasa kuhusu maadili ya familia. Sababu zake ni mchanganyiko wa mambo mengi ambayo ni vigumu kuyachambua katika barua fupi ya aina hii.
Ju,hudi za kurekebisha maadili zinahitaji msaada pekee wa Mwenyezi Mungu. Yeye akiwa jiwe la msingi wa jitihada zinazofanywa na watu wote wenye mapenzi mema, ni hakika kuwa tutajenga maadili yaliyo imara. Maandiko Matakatifu yanatuhakikishia neno hili yasemapo:
"BWANA asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji, yeye aulindaye akesha bure"[18]
Tena yanatueleza baraka kwa mtu mwadilifu:
"Heri kila mtu amchaye Bwana, aendaye katika njia zake, Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
Tazama atabarikiwa hivyo yule amehaye Bwana".[19]
Kumomonyoka kwa maadili kumejitokeza katika nyanja zifuatazo:-
UTAJIRI WA HARAKAI HARAKA
12. Iko tamaa kubwa ya kujitajirisha kwa haraka iwezekanavyo bila kujali vipengele vingine kama vile haki na kazi ngumu. Matukio ya upotevu wa.mali ya_serikali bila maelezo ya kuridhisha; wizi wa moja kwa moja; kuchelewesha au kupoteza mishahara ya wafanyakazi na mengine ya aina'hii ni upotofu unaofahamika. Sababu ya msingi ya tabia hiyo ni kufishwa kwa dhamiri ya mtu. Ile sauti ya ndani ya mwanadamu drayampaigma anapofanya lililo jema na kumkaripia anapofanya ovu imewekwa pembeni katika sekta nyingi za maisha. Tunaipongeza serikali kwa azma yake ya kuamsha moyo wa kuwajibika. Lengo hili litafanikiwa zaidi iwapo watu wanajisikia kuwajibika kutokana na msukumo wa ndani. Msukumo huo unatokana na uamuzi wa mtu kujituma kufanya jema na kuacha lililo ovu. Ha.sa.hasa sauti hi.i inamtuma mtu kutenda kulingana na hadhi ya kibinadamu, awe na tabia ya kibinadamu katika yale anayofanya - ndiyo kusema awe na dhamiri adilif u inayomwo¬ngoza. Kufurahia ambacho hukukitokea jasho ni kupingana na dhamiri iliyonyooka. Kutafuta maisha yaliyo bora ni hamu halali kabisa, lakini siyo sawa kufanya hivyo kwa njia zinazobomoa jamii au kukanyaga haki na heshima ya wengine. Kwa mfano tamaa ya mali ya haraka haraka pamoja na anasa vinaweza vikaleta madhara mengi kama vile kusababisha hongo, uonevu, kunyanyaswa na hata kudhalilishwa kwa binadamu.
ULEGEVU KATIKA KAZI
13. Kumejitokeza pia tabia ya utepetevu,kutozinduka katika wajibu tulizopewa. Mhusika anakaa kwa namna ambayo kufanikiwa au kutofanikiwa kwa wajibu fulani hakumwongezei chochote. Yu si moto wala si baridi! Mradi malipo mwisho wa mwezi. Matokeo ya tabia ya aina hiyo ni kwamba mhusika hanyumbuki katika utu wake wala hachangii maendeleo katika kazi yake. Kiasilia chimbuko la maendeleo ni mtu mwenyewe. Iko haja ya kuwaunda wahusika wenye wajibu wowote kujisikia kuwa wanachofanya ni chao na kinajenga utu wao; kufaulu au kushindwa ni kwao.
Kuhusiana na tabia tuliyoieleza hapo juu inatokea kwamba uwaji¬bikaji unasogezwa kwa kitu au half isiyo na "Unafsi" ili kukwepa kubeba lawama. Hiki ni kisingizio cha kukwepa wajibu. Ipo misemo kama "hali halisi", "sababu zisizoepukika", "umma", n.k. Umma ni watu jumiajumla tu, huwezi kuupeleka umma kortini. Ni kitu gani hiyo "half halisi"? Hakisemwi. Hizo sababu zisizoepukika ni zipi hasa? Zaweza kuwa kitu chochote - kizito au uzembe tu. Ingefaa kusema kikwazo chenyewe ili kiweze kutafutiwa njia ya kukiondoa. Je, kuna half halisi inayohalalisha upotevu wa fedha? Kwa nini tusiseme imepotea kwa kuibwa? Sababu gani treni..imechelewa? Kumbe dereva alichelewa kufika. Kufaulu au kutofaulu ka_tika hatua za kimaendeleo kiasi kikubwa kunategemea wale binadamu wanaotawala nishati zilizopo. Wao ni wa maana kuliko nishati zenyewe. Wakubali kuwajibika na kutoa hesabu. Wawe na dhamiri.
URASIMU USIOFAA
14. Tunapozungumzia urasimu tunamaanisha zile taratibu za kuunganisha shughuli za watu wengi kufanikisha jambo fulani wanalolifanya. Ili shughuli fulani zipate kwenda sawa sawa lazima kuwepo urasimu kiasi fulani. Lakini urasimu unapozidi, unakwamisha utendaji na pengine kukwamisha shughuli yenyewe. Matokeo ni kwamba urasimu katika sekta moja unakwamisha utendaji katika sekta nyingine zinazohusiana na hivyo kusababisha hasara kubwa ya upotevu wa mali na muda. Vile vile wenye nia njema wanakatishwa tamaa. Licha ya hayo, urasimu uliokithiri waweza kuleta kishawishi cha kutoa hongo - ubaya ambao umekuwa sugu katika sekta mbalimbali.
Mara nyingine wahusika wanachelewesha kutoa uamuzi bila sababu zilizo halali na hivyo kukwamisha hatua za kimaendeleo. Mhudumu anasema'"nenda urudi kesho" na kesho anarudia lile lile. Sababu za kusema hivyo anazifahamu mwenyewe! Uoo ulazima kwa viongozi kuwa watu wenye kauli na ujasiri wa ku toa uamuzi ulio na msimamo wa kweli. Wasipofanya hivyo wanajipotezea imani ya wale wanaohitaji huduma zao.
15. Kati ya hatua za kuondoa urasimu mbaya ni kuweka to zile taratibu zinazotakiwa; kua.iiri kwa kuwa kuna kazi, siyo kuajiri ili kuunda kazi; kuwa na wahudumu wenye uwezo wa kumudu kazi zao. Hao wawe wenye kuwajibika. Hapa tena ni suala la maadili yaani dhamiri kama ilivyoelezwa huko nyuma.
KUREKEBISHA HALI HIYO
Kufanya kazi kwa bidii
16. Mwenye kufanya kazi fulani iwe ya akili au ya kutumia musuli, anastahili heshima na matunda ya haki ya kazi yake. Kufanya kazi kunamwezesha mwanadaml,tnmkiiza nafsi yake pamoja na vipaji alivyojaliwa. Ni vigumu kumpata binadamu halisi ambaye hajisikii msukumo wa kufanya kazi. Lengo la kazi ni kujipatia mahitaji ya lazima ya kuishi hasa kuhifadhi uhai wa mtu. Kazi anayoifanya mtu ni mali yake kwa vile anatumia nguvu za nafsi yake. Kazi ni njia mojawapo tuliyowekewa tuweze kukua na kuwa binadamu kamili. Kinyume chake uvivu ni kukondesha utu.
17. Ingawa kazi anayoifanya mtu ni mali yake inamhusisha na jamii kutokana na uhusiano wake na watu wengine na mahitaji ya jamii. Tunaweza kusema taifa hukua kutokana na kazi wanazozifanya wazalendo wake.[20] Ili kazi iweze kumkuza yule anayeifanya inahitaji ifanywe kwa bidii na kujituma. Mungu anapomwumba mtu anamweka duniani iii amfanyie kazi fulani yeye binafsi. Asipoifanya yeye haitafanywa na mwingine. Kwa hiyo kila mwanadamu aliyejaliwa umri wa kufanya kazi achangie sehemu yake katika ulimwengu huu. Ni aibu kurudi kwa Mungu mikono mitupu. Ndani ya kila binadamu wa kawaida Mungu ameweka namna ya silika ya kushindana na mazingira ili apate kuyashinda na hivyo kufaulu na kutulia. Huu ni msukumo wa kufanya kazi kwa bidii. Pia yafaa kukumbuka kuwa kupokea malipo kwa kazi ambayo mtu hakuifanya au ameifanya hovyo ni ukosefu wa haki; ni wizi. Mungu mwenyewe ametuwekea sheria ya kufanya kazi kwa bidii aliposema: "Kwa jasho la use wako utakula chakula."[21] Sheria hii ni kwa kila mwanadamu mwenye nguvu za kufanya kazi. "Mtu asipofanya kazi na asile", atuambia Mtakatifu Paulo.
KUITIISHA DUNIA
18. Chimbuko la mema yote ulimwenguni ni tendo la Mungu la kuumba dunia na mwanadamu. Mwanadamu aliumbwa na uwezo wa kuitiisha dunia kwa kazi yake.[22] Dunia ambayo ni zawadi ya kwanza kwa mwanadamu inamtii mwanadamu na kumzalia matunda anapoifanyia kazi. Lakini dunia haimpatii kitu asipoipokea kama zawadi na kuifanyia kazi.
Kazi inamfa:a, mwanadamu kwa namna nyingine. Kwa njia ya kazi ambapo mwanadamu anatumia akili na uhuru wake, anabadilisha dunia na kuifanya iwe nyumbani kwake. Nchi yetu imejaliwa milima na mabonde, mapori na misitu, mito na bahari. Haya yote hayajatiishwa na sisi yawe mali yetu kwa kazi; ni kama hatujapokea zawadi Mwenyezi Mungu aliyotupatia. Sehemu kubwa ya umbile la nchi yetu ingali kama ilivyotoka mikononi mwa Mwenyezi Mungu; hatujaifanya iwe mali yetu kibinadamu ingawa iko chini ya bendera ya taifa. Inangoja juhudi zetu tuifanye iwe yetu kwa kazi.
19. Kabla ya kuendeleza tafakari hizi ni muhimu tukumbuke Kanuni moja ya kutuongoza. Nayo ni hii: Katika kuitiisha dunia ikumbukwe kuwa Mungu ameitoa dunia kwa jinsi yote ya wanadamu, siyo kwa mtu binafsi, au kwa kumpendelea huyu na kumnyima yule. Hili ndilo lengo asilia la mali yote ya ulimwengu.[23] Kwa'msingi huo si haki kumzuia fulani kutumia sehemu ya zawadi waliyopewa watu wote mradi azingatie taratibu za haki zilizowekwa na jamii.[24] Bila shaka anapaswa kufanya hivyo akishirikiana na wengine, na pasipo kuweka pembeni manufaa mapana ya jumuiya. Ndiyo maana inahitajika kuunda ushirika, kampuni na vikundi vya aina nyingine ili kazi ya kutiisha dunia ifanyike kwa ufanisi na manufaa ya wote. Kazi inayozaa matunda inadai mipango bora iliyo thabiti; nayo mipango inadai kuongozwa kwa nidhamu ya hali ya juu, kipawa cha kujiwekea malengo ya mbali, ujasiri na ari ya uvumbuzi. Hapa tunaona wazi kuwa mali asili ya msingi tuliyo nayo ni "Mtu Mwenyewe". Kichocheo na lengo la maendeleo yote hi binadamu. Akili yake inamwezesha kugundua nguvu zilizo katika maumbile na jinsi ya kuzitumia kwa manufaa yake na wengine. Kwa njia hii mwanadamu anakamilisha uwezo wake wa kuunda mazingira ya kibinadarnu.
20. Ushirikiano ni muhimu sana katika kazi. Daima Kanisa linahimiza kazi za kujitolea na kumwalika kila.mmoja ashiriki katika miradi ya pamoja. Ili kupunguza roho ya ubinafsi iliyomganda mwanadamu tunapasws kuendeleza matendo ya Fungamano na Upendo tukianzia na familia ambapo watu wanaishi pamoja na kutegemezana. Inaleta uchungu inapotokea kwamba wanafamilia wanapoamua kuishi vema wito'wao hawapati misaada sahihi na ya kutosha kutoka kwa jamii. Kwa hiyo inabidi kuendeleza siyo to maadili ya wanafamilia bali pia wale wanaosaidia kukuza familia bora. Wote wanapasika kusimika huduma zao katika taratibu zinazomjali Mungu na uhuru wa wanafamilia. Vilevile wanafamilia wanayo haki ya kutafuta ukweli na kuchagua kuufuata kuendana na dhamiri zao. Tunakazia malezi ya familia kwa sababu ndipo utamaduni wa taifa unajengwa, tena juhudi za kuleta maendeleo ya kikazi hufuata mfumo wa utama¬duni ulio katika familia. Akili, moyo wa kujituma, vipawa vya uumbaji, kujitawala, tabia ya kugawiana hutegemea sana malezi katika familia.[25]
21. Suala la mazingira linaungana sana na juhudi za binadamu za kuitiisha dunia. Hamaki ya utajiri wa haraka na uchu wa kutosheleza mahitaji mafupi mafupi vimekithiri'sana katika ulimwengu wetu. Binadamu anakuwa nA tamaa iliyozidi ya kuwa na mali na kuifurahia kuliko kuishi vema na kuikuza nafsi yake. Anajiachia kiasi ambacho anabomoa misingi ya mali asili ya dunia na hata kujiumbua mwenyewe kwa uharibifu mkubwa. Mifano wazi inayojulikana ni utumiaji wa madawa ya kulevya na uporaji wa mali. Chanzo cha kasoro hizi ni kule binadamu kutozingatia ukweli alivyoumbwa. Anapogundua uwezo wake wa kutawala dunia kwa kazi yake, anadharau mpango aliouweka Mungu Mfadhili wake. Anafikiri anaweza kuitawala dunia bila kujali masharti yaliyojengewa katika hiyo dunia. Badala va kushirikiana na Mungu Muumbaji, anajifanya yeye kuwa mungu na hivyo kuzusha fujo na uasi katika maumbile. Hali hii inajidhihirisha jinsi mwanadamu anavyojitendea yeye mwenyewe na viumbe vinavyomzunguka. Kasoro ni kwamba mwanadamu anaangalia ulimwengu kwa mawazo hafifu na finyu; anashindwa kuutazama ulimwengu kwa mshangao wa uzuri wake na hivyo asimtambue Mungu anayejijulisha kwetu kwa njia ya viumbe. Ndiyo sababu vitu vingi vya maumbile vinaharibiwa bila kugutuka. Ukweli ni kwamba tumepewa dunia tuitunze na kuipamba, siyo kuitumia bila akili na mpango.
22. Tunatambua juhudi nyingi zina zofanywa hapa nchini katika kuhifadhi mazingira na mali asili. Tunamwomba Mwenyezi Mungu abariki juhudi hizi zifanikiwe zaidi. Msukumo wa juhudi,hizi unatokana na seri¬kali hasa. Raia wa kawaida hawaoni kwa urahisi sababu ya maha¬ngaiko hayo yote. Wengi wao wanaendelea kuwaua wanyama pori, kuchoma moto misitu, kukata misitu bvyo n.k. Kazi kubwa ni kuamsha mawazo na kujenga tabia ya kuyapenda na kuthamini mali asili na mazingira mazuri. Mali asili na mazingira vithaminiwe siyo to kwa kuleta shibe na uchumi bali hasa kwa malengo ya kulea akili, kulisha moyo na kuinua roho. Inafaa mawazo haya yaingizwe katika malezi kuanzia nyumbani na kuendelezwa katika mpangilio wote wa elimu tangu shule za msingi mpaka vyuo vikuu. Vilevile jamii kwa jumla ielimishwe kwa kutumia vyombo vya mawasiliano, jambo ambalo lime¬kwishaanza.
23. Kuna sekta kadhaa ambazo tunafikiri zinahitaji hatua za, haraka zichukuliwe. Mojawapo ni maji. Chemchemi nyingi na vyanzo vya mito vinatoweka kutokana na kukata misitu na kulima mabonde kando ya mito. Sote tunafahamu kuwa uhai hauwezi kuendelea bila maji. Hatua kali na za haraka zichukuliwe ili kuhifadhi misitu inakoanzia mito na chemchemi. Sekta nyingine ni miji. Miji ni use wa utamaduni wa taifa lolote. Miji ni mahali ambapo watu wanajifunza uungwana na hali bora ya maisha. Kwa maneno mengine miji ni shule ya uraia mwema. Ili kuifanya miji iwe mahali pa kuvutia wenyeji wake wanapaswa kuji¬ husisha kuifanya miji yao iwe mahali pa kumstahili binadamu. Serikali , isisahau wajibu wake.
Sehemu ya Pili: FAMILIA CHIMBUKO LA MWANADAMU NA JAMII
Maingilio:
24. Uhai kadiri ya Imani yetu, ni zawadi ya Mungu kwetu. Uhai ni zawadi ya kwanza tunayopewa na Mwenyezi Mungu; bila kupewa zawadi hii kwanza hatuwezi kupokea zawadi nyingine kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Uhai duniani ni tunu-tegemezi ya kila kiumbe chenye uzima. Kwa upande wetu sisi binadamu ukweli huu unadhihirika zaidi[27] kwa sababu uhai wa binadamu umepewa thamani inayopita hadhi ya viumbe vingine vyote ulimwenguni. Thamani pekee ya uhai wa binadamu ni kwamba binadamu amekusudiwa kuunganika na Mungu katika heri ya mbinguni.
Uhai wa binadamu ni kazi ya Mungu inayotokana na rnpango wake wa milele katika kuumba. Lengo la kumwumba mtu anayelijua kikamilifu ni Mungu peke yake. Kwa hiyo binadamu kwa upande wake hawezi kuutendea uhai wake kama apendavyo.
Wajibu muhimu na ,nzito Mungu aliowakabidhi watu wa ndoa ni kushirikiana na Mungu katika kuleta uhai wa maisha mapya duniani. Lakini wajibu huu haukosi ugumu na matatizo yake, ingawa unakuwa pia chemchemi kubwa ya furaha na uperdo.
Siku hizi zetu vimekuwepo vikwazo vinavyohatarisha uhai na familia kutoka pande nyingi. Ndiyo maana tumelazimika kutoa kauli ya Kanisa Katoliki kuhusu suala hili lenye uzito wa kipekee kwa Wakristu na watu vote wanaonxaamini.Mungu., Kauli hii imehitajika sana wakati huu ambapo kuna mawazo mengi kuhusu familia, uzazi wa majira, malezi ya vijana, n.k. Tunaamini kuwa mwongozo huu utasaidia kuimarisha familia zetu za Kirristu na familia zote zilizosimikwa na Mungu, aliye Baba na chanzo cha familia zote duniani.[28]
MABIDILIKO KATIKA ULIMWENGU WETU
Mabadiliko mbalimbali katika ulimwengu wetu yamesababisha mawazo na mipango ya kdjihusisha na maisha ya ndoa na uhai wa mwanadamu kwa namna isiyomnufaisha mwanadamu na familia yake. Sababu zenyewe ni kama ifuatavyo:-
Mosi, ongezeko la watu duniani limeleta hofu. Hofu na woga ni kwamba watu wanaongezeka haraka kuliko uwezo wa uchumi wa kuwalisha.[29] Hivyo watu wa ndoa wanashauriwa wapunguze idadi ya watoto wanaopenda kuzaa, watawale kizazi kwa njia zozote bila kujali imani na maadili yanayomfaa mtu. Hofu na mahangaiko hayo yamezusha matendo ya hatari ya kujipatia majibu mepesi ya haraka pasipo kuangalia hali yote ya mtu mzima. Vilevile wataalam wameshawishika kupendekeza teknolojia za kupunguza kizazi au kuzuia kabisa, bila kuangalia hatari zinazotokana
na teknolojia hizo katika uwanja wa maadili ya wale wanaozitumia.
Tatizo la pili limetokana na hali ngumu ya uchumi. Familia nyingine hazina uwezo wa kutosha kutunza watoto wengi na kuwapatia malezi bora inavyotakiwa. Inashauriwa kuwa njia maalum ya kushinda tatizo hill
ni kupunguza watoto kama ilivyoelezwa hapo juu.
Tatu, kwa namna ya pekee mwanadamu wa leo anajisikia anao uwezo mkubwa sana kwa njia ya sayansi. Anajisikia anao uwezc juu ya mwili wake yeye mwenyewe na nguvu zake mbalimbali kama vile akili, utashi, jamii, licha ya uwezo wa kutawala viumbe vingine visivyo na roho. Anashawishika kwa urahisi kutumia ujuzi wa sayansi katika nguvu za uzazi pasipo kuangalia kwa makini nyanja nyingine za maisha ya mtu. Hapo sayansi inapotumiwa pasipo kuweka maanani maadili ya binadamu ina¬mietea binadamu madhara upande fulani.
Nne, maendeleo'ya kisasa na kukua kwa hadhi ya mwanamke kumetupatia mwanga wa kuelewa zaidi maana ya mapendo katika ndoa na nafasi ya mwanamke katika familia na jamii. Kanisa linafurahi na kutiwa moyo linapoona akina mama wanafurahia haki za kibinadamu na kupewa nafasi -ya kutumia vipaji vyao katika jamii. Lakini si mara chache mabadiliko haya yanagusa hadhi ya mwanamke kama mama katika familia.
Mambo haya na mengine mengi yameleta mtazamo tofauti mintnrafu Utakatifu wa ndoa, familia, thamani ya uhai n.k. Kwa sasa upo umuhimu wa kuyachunguza katika mwanga wa Ufunuo wa Mungu na mafunditho ya Kanisa. Kwa hiyo Kanisa ambalo ni Mwalimu wetu rasmi na Mama-Mleii Mkuu linapenda kutoa msimamo wa maadili kuhusu masuala haya yanayotugtsa sana kimaisha.
UHAI KATIKA MILA NA UTAMADUNI WETU
26. Babu zetu walithamini sana uhai, wakauheshimu na kuulinda kwa miiko mbalimbali ya kimila. Mwafrika anatamani kuishi alipo duniani na aendelee kuishi katika kizazi chake baada ya yeye kufa. Waafrika wa jadi waliona kupata watoto ni kuendelea kuishi. Kukosa watoto ni kukatika -balaa kubwa mno liwezalo kumpata mtu. Kwa hiyo familia na ndoa vililindwa kwa sababu ndiyo njia ya kuendeleza kizazi. Kwa Mwafrika, mama mwenye mimba aliheshimiwa na kutunzwa vizuri; hata makabila mengine walimwita "Mama mwenye Baraka".
Watoto walipokewa kama zawadi na baraka pekee kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hivyo walipendwa na kulelewa vema ili waweze kuendeleza jina .la wazazi na ukoo wao. Mtu asiyependa watoto na kuwathamini alione¬kana kuwa adui wa jamii.
Malezi ya watoto na vijana yalipewa uzito pekee kwani wao ndio baba na mama wa kuchukua nafasi ya wazazi wao. Vijana waume kwa wake walipea malezi ya siri ya kuwaandaa wawe wazazi wa baadaye. Wavulana kadiri ya umri wao, walipewa malezi peke yao na baba mwadilifu aliye¬chaguliwa na jamii kwa wajibu huo. Hali kadhalika wasichana walifunzwa peke yao siri za umama na mama aliyekubalika mbele ya jamii. Hawa wakufunzi walitazamiwa wawe watu wenye sifa nzuri na maadili mema kwa jamii.
Vijana hao walifundishwa maadili ya mume na mke, malezi ya watoto na mwenendo mwema katika jamii na watu wazima. Walifundishwa pia njia za kupanga uzazi zilivyokuwa zinatumiwa na wazee wao walivyozipokea toka babu na bibi na kuendelea mpaka babu wa mababu na bibi-wazee wa zamani. Namna yao ya kupanga uzazi.ilikuwa kutumia njia ya asili. Kwa njia hizo waliweza kupanga mtoto mwingine azaliwe baada ya mpaka miwili au mitatu, kadiri walivyoona inafaa.
Ingekuwa vizuri kwa kizazi chetu kujifunza hekima za mababu zetu na kuendeleza yale mazuri waliyokuwa nayo kuhusu familia na malezi ya watoto. Yale yasiyopingana na sheria ya Mungu yaendelezwe badala ya kuiga mambo mengine ya kigeni yasiyol-ingana na maadili yetu.
UHAI KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU
Uhai Hutoka kwa Mungu
27. Imani yetu na imani ya dini nyingine hata ile ya wazee wetu zinathamini uhai wa mwanadamu kwa sababu zinabainisha na kushikilia kuwa uhai huo unatoka kwa Mungu. Biblia yetu sisi Wakristu hutuambia toka mwanzokwamba mwanadamu ameumbwa na Mungu inaposema:
"Mwenyezi Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia katika mianzi ya pua pumzi ya uhai"[30] Somo hili linaeleweka kwamba mavumbi ya ardhi ni mwili wa mwanadamu. Pumzi aliyopulizia Mungu ni roho ya mwanadamu inayoumbwa na Mungu aliye roho, wakati ardhi ni sehemu inayochangwa na baba na mama-mtu.
Waandishi wa Biblia wanadhihirisha mahali pengi kuwa pumzi ya uhai ni thawabu au paji la Mungu kwa wanadamu na viumbe vingine vyote. Isaya anasema: "MWENYEZI Mungu anena, yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda, yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu ya nchi; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake".[31] Mtakatifu Paulo anatuongelea neno hilo hilo asemapo.: "Mungu Mwumba wa ulimwengu na vyote vilivyomo, ni yeye mwenyewe ndiye aliyewapa watu uhai, anawawezesha kupumua na anawapa kila kitu".[32]
Mungu basi ni shina la uhai vote; ndiye aliyeuwekea :taratibu za kuudumisha na kuuendeleza; ndiye mwenye mamlaka yote juu ya uhai wa aina yoyote. "Fahamuni sasa ya kuwa, Mimi, naam, Mimi ndiye, wala hapana Mungu mwingine ila Mimi., Naua Mimi, nahuisha Mimi. Nimejeruhi, tena naponya,; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu".[33]"Mwenyezi Mungu huua, tena huleta juu".[34] Hivyo mwanadamu hana mamlaka juu ya uhai wa mwanadamu mwingine, kwani Mungu amempa amri: "USIUE".[35]
Binadamu Anashirikishwa Uumbaji
28. Mwenyezi Mungu ametaka.kumshirikisha mwanadamu kazi maarufu ya kutoa uhai, kuukuza na kuuhifadhi. Heshima hiyo amewajalia watu wa ndoa tangu awali kama baraka na amri. "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfar wa Mungu alimwumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba. Mungu AKAWABARIKI, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha".[36]
Kushirikishwa katika kuutoa na kuuhifadhi uhai ni kazi inuhimu sana na ya heshima kuu kwa binadamu. Katika kupatikana watoto nguvu tatu zinaunganika; nguvu ya baba, nguvu ya mama na Mungu mwenyewe. Utaratibu wa kuunganisha nguvu hizi ameuweka Bwana Mungu. Ni wajibu wetu sisi viumbe vyake kuuheshimu, kwa vingine tunamkosea Mungu na kujipatia madhara yasiyo na mwisho.
Baraka ya Kupata Watoto
Kupata watoto ni tendo linalounganika na matendo ya upendo kati ya wenye ndoa. Watoto huimarisha umoja kati ya baba na mama. Watoto ni chemchemi ya furaha na faraja kwa wazazi, yasemavyo maandiko matakatifu:
"Watoto ni zawadi itokayo kwa Mwenyezi Mungu, ni kama mishale mikononi mwa askari. Heri mtu aliyelijaza podo lake mishale hiyo kwa wingi, hatashindwa akishtakiwa na adui mahakamani".[37] Ni fahari kuona jumuiya ina wazee na watoto wengi kadiri ya fikra za Waisraeli na za Waafrika.
"Mwenyezi Mungu asema hivi: Wazee wanaume na Wazee wanawake watakaa tena katika barabara za Yerusalemu, kila mtu ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni wazee sana. Na hizo barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wakicheza katika barabara zake".[38]
Somo hili linatuashiria kuwa wale wanaopenda watoto watajaliwa maisha marefu na furaha ya kuwaona vijana katika uzee wao.
MWONGOZO WA KANISA KATOLIKI[39]
29. Tunapofikiria suala la kupanga uzazi inabidi tuliangalie kwa kuhusisha mtu mzima; tukwepe kishawishi cha kuegemea upande fulani kama vile Biologia au Psikologia; Demographia au elimu fulani ya jamii. Daima tumfikirie binadamu kama kiumbe wa hapa duniani na kiumbe mwenye wito wa kufikia maisha ya milele. Kanuni hii ni muhimu sana.
Kwa vile wale wanaohalalisha mpango wa uzazi kwa njia ya vyombo na madawa wanatetea kwamba mtindo huo unadumisha upendo katika ndoa, na pia unatoa fursa ya uzazi kwa kuwajibika, inabidi tueleze kwa undani maana kamili ya kweli hizi mbili zilizo nguzo za ndoa.
(1) MAPENDO KATIKA NDOA
30. Uhusiano wa ndoa si jambo lililozuka kwa bahati nasibu. Upendo wa ndoa umetoka kwa Mungu ambaye kwa asili yake ni Upendo[40] Yeye ni Baba ambaye kwake kila familia mbinguni na duniani inatajwa.[41] Katika ndoa ambapo mume na mke wanaunganika kuwa mwili mmoja, na ni muunganiko huu to ulio halali, hawa wawili wanapeana nafsi zao, wapate kuendeleza na kukamilisha maisha yao. Kwa kuunganika vile, wao wanashirikiana na Mungu katika kazi ya kuleta uhai mpya duniani! Kuna ukweli mkubwa zaidi. Ndoa ya waliobatizwa ina hadhi ya Sakramenti, ndiyo ishara wazi ya neema na kielelezo cha muungano kati ya Yesu Kristu na Kanisa lake Takatifu.
Mapendo ya ndoa ni upendo kati ya mtu-mume na mtu-mke, wakipendana katika half ya utu wao unaoshika mwili, roho na jamii. Upendo huu umesimikwa katika mtu kukubali kwa hiari kumpokea mwenzake kama mwenzi wa ndoa katika furaha na taabu mpaka kufa. Ndoa haitokani na kujisikia to au silika.
Ni upendo wa kuwa mwaminifu mpaka kufa. Uaminifu huu unaweza ukawa mgumu sana lakini una hadhi na furaha yake ya kipekee. Ni upendo wa kujitoa wote knbisa, namna ya urafiki mkuu kati ya wawili ambapo mume na mke wanashirikishana kila kitu cha maisha yao. itayempenda kweli mwenzake wa ndoa anafikiria furaha ya huyo mpendwa kuliko furaha yake mwenyewe. Wenye ndoa.wanatajirishana kwa kupeana upendo wao. Ni upendo wa kuthamini mwingine alivyo kuliko kuhesabu kinachopatikana kwake. Upendo huu unarutubisha, yaani unaleta baraka ya uzazi. Kwa maneno mengine umoja wa ndoa umeumbiwa ndani yake ujiendeleze katika kuzaa na kulea watoto. Vatikano ya Pili inatuambia; "Kwa asili yake mapendo ya ndoa yamepangwa kuzaa watoto, kwani watoto ni tunda kuu la ndoa; na hao watoto wanaimarisha usitawi wa wazazi wao".[42]
(2) Uzazilae Kuwajibika (Uzazi wa Majira)
31. Mapendo ya ndoa yanawahi,.izaa mume na mke watambue ukubwa wa wito wao. Siku hizi uzazi kwa kuwajibika unasisitizwa pande nyingi jambo ambalo ni zuri linapochukuliwa kwa usahihi. Yako mambo muhimu ya kuzingatia katika uzazi kwa kuwajibika;
1. Katika upande wa biolojia mtindo huu unadai kuelewa sawasawa na kuheshimu mtiririko wote wa paji la kuzaa ulivyowekwa kibiologia. Akili ya binadamu imeweza kugundua sheria ambazo ni sehemu ya umbile la mtu. Sheria hizi ziheshimiwe.
2. Paji la uzazi ni mojawapo ya nguvu zenye tabia ya silika katika binadamu. Uzazi kwa kuwajibika unadai binadamu atumie akili na utashi wake kujitawala. Silika iongozwe na akili na utashi.
3. Tukiangalia upande wa uchumi na elimu zingine za jamii, inapasa mtindo huu uamuliwe na wazazi wenyewe kulingana na imani na dhamiri zao. Ni wao wanaamua kupata watoto wengi, au kukwepa mazingira ya kupata mtoto mwingine kwa kipindi walichoamua, kutokana na sababu nzito na daima kujali sheria ya Mungu.
4. Unadai mume na mke watambue wajibu wao kwa Mungu, kwao wenyewe, kwa familia yao, na jamii - hayo yote katika ngazi ya uzito wake. Wanapoamua haya wawe na dhamiri zinazoongozwa na maadili mbele ya Mungu.
Kwa hiyo watu wa ndoa hawana uhuru wa kujiamulia to kama wangekuwa mabwana wa nguvu ya uzazi. Wanapaswa kuheshimu taratibu za mtiririko uliowekwa na Mungu. Utaratibu huu unaitwa Kupanga Uzazi kwa Njia ya Asili. Ndio mtindo inaokubalika na Kanisa.
(3) KUTEKELEZA MPANGO WA UZAZI WA MAJIRA KWA NJIA YA ASILI
32. Ikumbukwe daima kuwa mtu si bwana wa maisha na uhai wake, bali yeye ni mtumishi wa kutekeleza mpango wa Mungu. Maana yake mtu hana uwezo wote juu ya mwili wake na vipawa vyake. Heshima yote aliyotupatia Mungu ya kushirikiana naye kuleta maisha mapya duniani, wajibu huu hauwezi kuachwa to utekelezwe kwa kufuata uamuzi wa kila mtu peke yake, au kikundi cha watu peke yao bali lazima kutolewe mwongozo dhahiri wa Mama Kanisa, aliyekabidhiwa kazi ya kulinda na kufafanua kweli za maadili..[43]
1. Kanisa linaafiki na kufundisha mpango wa uzazi wa majira kwa kutumia njia ya asili.
2. Katika ndoa, si halali mwenzi wa ndoa kumlazimisha mwenzake kutumia ndoa bila kujali half ya mwenzake na kukubali kwake. Tendo la namna hiyo ni kinyume cha upendo wa,ndoa. Kufanya hivyo ni kuharibu uhusiano kati ya mume na mke. Vilevile ieleweke kwamba, tendo la ndoa linalofanywa kwa namna ya kuzuia uwezekano wa kupatikana kiumbe kipya, linapingana na mpango wa Mungu katika ndoa. Kutumia ndoa, zawadi hii ya Mungu, kwa kupingana na lengo lake ni kuharibu maana ya ndani ya ndoa; ni kwenda kinyume cha mpango wa Mungu na mapenzi yake kuhusu ndoa.
3. Tendo lolote la kuzuia mimba, kabla au wakati linapofanyika tendo lenyewe, au baadaye, ni tendo haramu lisiloruhusiwa kamwe na msimamo wa Kanisa.
4. Uzazi wa Majira ni neno muhimu kwa watu wa ndoa kadiri ya mafundisho ya Kanisa. Mama Kanisa anafundisha na kuruhusu Uzazi wa Majira kwa Njia ya Asili, yaani wenye ndoa kutoitumia kipindi cha kuweza kutunga mimba.. Lakini Uzazi wa Majira kwa njia ya kutumia vyombo au madawa, uwe umefanyika kwa kukubaliana wote wawili, au kinyume cha mmoja wao, unapingwa kabisa na Mama Kanisa. Sababu ni kuwa unaingilia maumbile ya tendo la ndoaulilivyowekwa na Mungu.
5. Kuharibu uhai mpya uliokwisha anza (kutoa mimba) ni uhalifu mkubwa sana; ni tendo baya sana la kuua.
6. Kufunga kizazi kwa namna yoyote au njia yoyote ile ni kupingana na Mungu katika mpango wa kuumba; ni kwenda kinyume cha maumbile. Matibabu ya magonjwa lakini, hata kama matokeo yake yatazuia uzazi, hayapingani na mafundisho ya Kanisa.
(4) Athari za Vizuia Uzazi (Vyombo na Madawa)
33. Uzazi wa Majira kwa njia ya madawa unaweza ukahatarisha umoja wa ndoa kirahisi sana.
1. Uaminifu katika ndoa unahatarishwa
2. Maadili ya ndoa yanapungua
3. Hadhi ya mwanamke inashuka; anatumika kama chombo
4. Tendo la ndoa linapoteza hadhi yake ya kueleza uhusiano kati ya binadamu
5. Nguvu za uzazi zinatumika ovyo pasipo kujali mipaka na malengo yake
6. Hali hiyo inafungua mlango kwa matatizo mengi; magombano, chuki, magonjwa n.k.
7. Mtu anapoteza kuona na kuelewa maana ya uhai wa binadamu na lengo lake.
(5) Neno kwa Viongozi
34. Tunatiwa moyo kwa juhudi zinazofanywa na viongozi mbalimbali ili kuimarisha desturi nzuri za maadili katika taifa letu. Pamoja na kutambua juhudi hizi, imetubidi pia tutoe neno la angalisho kwa wale wote wanaoshughulikia elimu na malezi ya vijana, utamaduni pamoja na usitawi wa jamii kwa jumla. Tunawatafadhalisha wasikubali maadili ya nchi yetu yatiwe aibu ama kuvurugwa. Wasikubali zipitishwe sheria zinazopingana na haki na misingi ya binadamu. Familia ambayo ni msingi wa uhai na shina la taifa zima, isiingiliwe kwa mipango inayopingana na kanuni za maumbile au sheria ya Mungu. Katika kuangalia ongezeko la watu wawe na hekima ya kujali maadili ya familia pamoja na kuheshimu haki na uhuru wa kila raia.
(6) HIMIZO LA KICHUNGAJI
35.1. Kanisa, ambalo ni Mama na Mwalimu wa watu wote linopotoa tamko kuhusu tatizo fulani, linatoa msimamo wake kwa uaminifu mkubwa kwa Mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristu, kwa sababu kusudi la Kanisa'kuwako duniani ni kutusaidia sisi sote tupate kufikia maisha ya uzima wa milele. Hili ndilo lengo lake vilevile linapotoa mwongozo juu ya Uzazi wa Majira.
2. Kanisa linataka watu wa ndoa watambue kwamba maisha ya familia yana baraka na neema kubwa kwa wenye kufuata uzazi wa majira kwa njia ya asili. Mpango huu unawapatia mume na mke nafasi ya kuweza kujenga fadhila za kujitawala, sadaka ya upendo na kumtegemea Mungu anayewawezesha kutimiza wajibu wao.
3. Wazazi Wakristu inawapasa hasa katika kipindi hiki cha mawimbi na misukosuko, kwa nguvu ya neema walizojipatia katika.Sakramenti ya Ubatizo na Ndoa, kuzingatia wajibu zao hizo. Wanapozitimiza wapate kuwa kweli chumvi na chachu katika ulimwengu na kumshuhudia Kristu siku zote.[44]
4. Wazazi Wakristu wajitahidi kubeba mzigo wa wito wao kwa moyo wa Imani inayotegemezwa na Sala na Komunyo Takatifu. Pale wanapo¬shindwa kwa ajili ya udhaifu, wasikate tamaa, bali wamrudie tena Mungu kwa Sakramenti ya Upatanisho. Kwa njia hiyo watu wa ndoa wanaweza kujipatia na kufikia ukamilifu wa utakatifu waliotayarishiwa katika wito wao.
5. Amri ya Tano ya Mungu inasema "USIUE". Hii niamriasiyo shauri.¬ Hivyo uhai wa mtu ni kitu cha kujali sana kwakila mmoja wetu. Uhai wa Mtu,,,kwa upande mmoja, rii kazi ya Mungu katika mtu, kwa kuwa Mungu ndiye Mwumbaji wa vitu vyote. Kwa uoande mwingine, uhai wa mtu ni kazi ya mtu, kwa maana kwamba ni jibu la mtu la kumtii na kushirikiana na Mungu katika kazi hii ya kuumba.
6. Katika Amri ya Tano ya Mungu, Mungu mwenyewe anatufundisha wajibu wetu wa kutunza huo uhai tuliokubali kushirikiana naye katika kuumba.

7. Siyo hivyo tu. Kila mtu anapaswa kutunza uhai wake (maisha)na kujiendeleza aweze kufikia kikomo chake. Kutokana na fundisho hili haturuhusiwi:

- Kufanya kitu kinachoharibu uhai wetu na kuupoteza moja kwa moja;
huku ni kujiua mwenyewe
- Kui:ata viungo vya mwili; Tendo lolote la kupunguza au kuharibu-viungo vya mwili wako au wa mwingine si halali, isipokuwa kuna sababu nzito, kama ugonjwa.
Hairuhusiwi kabisa kuangamiza maisha ya mwingine, hata wakati akiwa katika tumbo la mama yake, iwe imetungwa mimba kwa njia ya halali au la. Kufanya hivyo ni kuua mtu. Mungu amekataza hilo.
Sehemu ya Tatu: NCHI YETU LEO NA KESHO: TANZANIA KUELEKEA MWAKA 2000
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu:
36. Katika sehemu hii tunapenda.kutoa taswira ya nehi yetu tunavyoiona kwa mtazamo wa Ufunuo wa Mungu na fikra za Kanisa Katoliki. Katika fikra za Kanisa "Mtu Mwanadamu" aliye mwili na roho, aliyepangiwa maisha ya hapa duniani na maisha ya milele mbinguni, ndiye dira ya kupimia maendeleo ya kijamii ya kisiasa na ya kiuchumi.[45] Fikra zifuatazo zitatilia maanani mabadiliko makubwa tunayoingia kwa kukubali mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukua kama taifa kwa hatua za amani, umoja na uhuru kwa kipindi cha miaka thelathini iliyopita. Kwa kipindi hicho kumekuwepo juhudi za kumjenga Mtanzania kwa kutumia misingi ya kujal.i haki za binadamu, mojawapo muhimu sana ikiwa ni uhuru wa kila mtu kuamini anavyoongozwa na dhamiri yake. Madhehebu yamepewa uhuru wa kutekeleza huduma zake za kidini kwa amani, pamoja na kuchangia maendeleo ya watu kwa jumla. Tunatambua kuwa hizi ni baraka kubwa. Hivyo tunatoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu na kwa wote wanaohusika. Kwa kusema hivi hatuna nia ya kutathmini yote yaliyofanyika katika sekta mbalimbali za jamii, la pasha. Nia yetu ni kutambulisha ile misingi maalum ambayo imekwisha kuwa nguzo za maendeleo ya nchi yetu. Kwa kweli bila kuwa na nguzo hizo tungekuwa tumepungukiwa sana. Hapa hapa mwanzoni inafaa tusisitize tena ukweli wa Kanisa kwamba, kwa mtu binafsi au jamii ya watu, zaidi ya kupata yale yanayotosheleza mahitaji ya mwili, annhitaji tunu za kiroho na za kiimani, kwani "MTU HAISHI K14A MKATE TU ILA, kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu".[46]
Mienendo Tuliyoji jengea Tangu Uhuru:
37. Tukiangalia historia ya nchi yetu tangu tulipojipatia uhuru, tunagundua tabia au mieneudo ambayo inamfanya Mtan ania alivyo, yaani Mtanzania halisi. Kwa kifupi mienendo hiyo ni kama ifuatavyo:
1) Tumejipatia uhuru kwa njia ya majadiliano na uclewano pasipo vita. Njia yetu tango mwanzo wa uhuru imekuwa ni ya kutumia hoja za kuri,ihisha, siyo mabavu
2) Tumejijengea umoja wa kitaifa pasipo kuegemea dini yoyote, kabila au kanda. Hii ni njia ya haki na usawa wa raia wote. Sisi ni Watanzania, na hii ndiyo fahari ya uzalendo wetu sasa.
3) Tumepitia mabadiliko mengi na makubwa bila kufarakana, wala mgongano wa kuumizana. Tabia yetu imekuwa ya kusikilizana kwa uvumilivu na utulivu mpaka kufikia uelewano na uamuzi.
4) Chama na Serikali hadi leo havifungamani na dini yoyote ingawa kila raia ana uhuru wa kufuata dini anayoamini. Msingi bora sana!
5) Nchi yetu inaheshimu sana haki za Binadamu kulingana na Katiba ya Umoja wa Mataifa. Sisi wenyewe tunazingatia haki hizo kwa kuwa tunazielewa na kuzithamini
6) Tunathamini uhuru wetu kiasi kwamba tunachangia kwa half na mali ili uhuru upatikane popote barani Afrika na penginepo.
7) Nchi yetu inathamini na kulinda amani na utulivu katika mienendo yake. Tunapotatua matatizo yetu daima tunatumia majadiliano ya amani mpaka kufikia uelewano. Tunatumia akili kwa hoja zenye kweli na haki; kamwe hatufuati mkondo wa chuki, upendeleo au nguvu.
Hizi ndizo baadhi ya tabia tulizojiundia. Ni muhimu sana kuzilinda, kuzidumisha na kuziendeleza.
Demokrasia kwa Njia ya Vyama Vingi
38. Baada ya kusema haya tungependa kuongeza machache mintarafu uamuzi wa kuendeleza Demokrasia kwa njia ya vyama vingi. Maoni yanayoto¬lewa hapa ni mchango wa Kanisa wa kusaidia kwa kiasi fulani nia njema za viongozi wanaohusika katika ngazi mbalimbali.
Kanisa linathamini mpango wa demokrasia kwa maana kwamba raia wana¬shiriki katika kuamua mambo ya siasa, inatoa nafasi ya kuchagua viongozi wanaofaa kuongoza serikali, na kuwabadilisha kwa njia za amani inapofikia wakati wa kubadilisha. Kamwe Kanisa halikubaliani na uundaji wa vikundi vidogovidogo vinavyojinyakulia madaraka ya kiserikali kwa malengo ya ubinafsi au kwa lengo la kulinda itikadi fulani fulani.[47]
Baba Mtakatifu Yohani Paulo wa Pili anasema hivi juu ya vemoxraz~.La.¬"Demokrasia halisi inawezekana to katika serikali inayotawala kwa sheria kwa misingi sahihi ya kumwelewa mwanadamu. Inadai yawepo mazingira ya kumwendeleza mtu binafsi kwa kumwelimisha na kumlea katika tunu zenye ukweli, pamoja na kuunda jamii yenye vyombo vva kushirikisha watu kwenye madaraka. Ifahamike kwamba shughuli za kisiasa zapaswa laislmEoa. katika kweli zilizo thabiti. Historia imeonyesha wazi kuwa Demokrasia isiyokuwa na tunu zilizo thabiti inageuka kwa urahisi kuwa serikali inayojichukulia kila kitu (Totalitarianism), au serikali ya mabavu iliyojificha"[48]
Baba Mtakatifu anaendelea kusema:
"Wala Kanisa halifungi macho yake kwa kutoona athari za ushupavu wa kushikilia kama imani fikra fulani fulani (fanaticism), au kutegemea kanuni za asili (fundamentalism). Wanaofuata fikra hizi wanalazimisha wengine wakubaliane na mawazo wanayojidai ndiyo ukweli wenye manufaa kwa wote. Ukweli wa Kikristu si wa namna hiyo. Imani ya Kikristu siyo itikadi inayoziba uwezekano wa mabadiliko. Inatambua kuwa maisha ya mtu yanaendelezwa katika mazingira yanayo¬ badilikabadilika Njia ya Kanisa daima inaheshimu uhuru".[49]
39. Kutokana na haya yaliyosemwa juu ya Demokrasia tunashauri ifuatavyo:¬
- Uongozi wowote utakaoshika madaraka uwe na dhamiri nyofu ya kutumikia wananchi wanaowachagua. Siku zote uongozi uheshimu tunu zetu za kitaifa.
- Wenye kushika madaraka wawe na tabia ya ukadiri ya kuvumilia wengine kujitokeza kwenye uwanja wa siasa. Hii ifanyike bila kuzusha vurugu katika jamii. Mambo yafanyike kwa uwazi, haki na ukweli.
- Kwa vile watu ndio taifa na ni wao wenye kuchagua viongozi wao, iko haja ya kuwaelimisha watu wafahamu kinaganaga wanachotaka taifani, na ni viongozi wa aina gani watawatimizia matazamio yao. "Wawe na mwamko wa kisiasa wasije wakadanganywa na wakorofi wanaotafuta madaraka kwa faida yao. Elimu kwa wananchi ni muhimu sana.
- Usawa wetu uchukuliwe kwa magna ya watu vote kuwa na haki zilizo sawa kutokana na.hali ya kuwa mtu, siyo usawa wa kusawazisha, kwani watu wana vipawa tofauti. Iwepo nafasi ya watu binafsi kujiendeleza kiuchumi kwa manufaa yao na jamii. Nafasi hiyo ikikosekana wale wenye uwezo wataLufa moyo na kujiondoa kwenye uwanja wa siasa na maendeleo.[50]
- Maendeleo yanayomjenga mtu kimaadili yapewe uzito wa kutosha. Maendeleo ya kiuchumi to ni ya upande mmoja, hayatamfaa mwanadamu kikamilifu yasipokamilishwa na ukomavu wa dhamiri na kuwajibika.
Mwaliko kwa Walei:
40. Katika barua hii ya Kichungaji, tunapenda kuwaalika Wakristu Walei wote waingie kabisa katika shughuli za Kanisa. Utume wao uanzie kwenye familia na kuimarishwa katika Jumuiya ndogondogo za Kikristu. Jumuiya hizi zienezwe na kudumishwa kila mahali penye Wakristu. Walei wasijifikirie kuwa wao ni wanakanisaa tu, bali ni sehemu kubwa ya Kanisa lenyewe.
Kwa hiyo wakati huu tunapojiandaa kufikia mwaka wa 2000 walei mjiandalie mipango maalum na kushirikiana na wanakanisa wengine, jinsi mtakavyotimiza utume wenu, ikiwa ni pamoja na kuwarithisha vijana na watoto mila na desturi zilizo njema. Kuweni Wamisionari kwa mwenendo wenu mwema, matendo yenu yawe mwanga kwa watu wote wapate kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.[51]
Vilevile msisimko wa Katekesi ambayo inajishughulisha kupata wafanyakazi katika shamba la Bwana;uwe ni wito wenu pia. Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke wafanyakazi katika mavuno yake.[52]
Tunatazamia kuwa utume wa walei utatekelezwa katika sehemu na sekta zote za'kazi na utumishi wa jamii. Utume huo basi uwe ni chumvi na chachu katika nyanja mbalimbali kama vile: uchumi, Siasa, uongozi, kilimo, biashara, elimu, afya, malezi na maadili bora.
Unjumbe kwa Vijana
41. Tunapenda kuwahakikishia vijana kuwa Kanisa linawapenda na kuwathamini sana. Shida zenu ni zetu, matumaini yenu ni matumaini ya Kanisa. Tuna imani kubwa na nguvu na uwezo wenu. Huu ndio wakati wa kujenga Imani yenu, maadili bora, na tabia ili muweze kukomaa zaidi. Mafanikio ya baadaye ya taifa letu yatategemea sana .luhudi. maarifa na maandalizi yenu ninyi vi jana . Hivyo tunawaalikeni, mjishirikishe katika mipango yote ya Kanisa. Tumieni nguvu na karama zenu kwa kufanya kazi kwa bidii ili mjipatie mahitaji ya kila siku. Tunawaasa mjiepushe na yale yote yanayoharibu utu na heshima ya binadamu. Mwisho tunawaombeeni Baraka za Mungu.
MWISHO:
42. Barua yetu hii imeandikwa kwa nia njema na matumaini makubwa kwamba tukiwa pamoja tunaweza kuleta maendeleo bora yatakayomletea kila Mtanzania maisha ya kheri, furaha na amani. Ni mwaliko kwa kazi ngumu kwa kila mmoja wetu. Ni wajibu wetu kujipatia heri hiyo, kwani uwezo tunao. Lakini hatutafikia lengo hili bila ushirikiano mkubwa na nia nyofu. Dunia yetu inatamani sana watu waishi pamoja kwa udugu. Utengano ni adui wetu mkubwa.
Tunamalizia kwa kuwaombea wote Baraka ya Mwenyezi Mungu:¬
Mwenyezi Mungu ndiwe shina la upendo;
Waimarishe watu wako watoe ushuhuda wa Injili kwa wanadamu wote; Leta Mwanga wa ukweli pale penye giza;
Leta nguvu penye woga na unyonge;
Leta upendo penye chuki;
Imarisha haki penye uonevu;
Dumisha Amani, Haki na Uelewano;
Utujalie haya kwa usitawi wa jamii yote ya Tanzania.
Imetolewa Pentekoste, tarehe 7 June, 1992 Dar es Salaam. Ni sisi Maaskofu wenu,
1. Mhashamu Askofu Josaphat Lebulu, wenyekiti
2. Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa
3. Mhashamu Askofu Mkuu Marko Mihayo
4. Mhashamu Askofu Mkuu Mario A. Mgulunde
5. Mhashamu Askofu Mkuu Anthony Mayala
6. Mhashamu Askofu Mkuu Polycarp Pengo
7. Mhashamu Askofu Holmes Sielde
8. Mhashamu Askofu Charles Msakila
9. Mhashamu Askofu Renatus Butibubage
10. Mhashamu Askofu Vincent Dennis Durning
11. Mhashamu Askofu Gervasius Nkalanga
12. Mhashamu Askofu James Sangu
13. Mhashamu Askofu Adrian Mkoba
14. Mhashamu Askofu Bernard Mabula
15. Mhashamu Askofu Christopher Mwoleka
16. Mhashamu Askofu Maurus Komba
17. Mhashamu Askofu Raymondo Mwanyika
18. Mhashamu Askofu Nicodemus Hhando
19. Mhashamu Askofu Mathias Isuja
20. Mhashamu Askofu Nestor Timanywa
21. Mhashamu Askofu Castor Sekwa
22. Mhashamu Askofu Beranrd Ngaviliau
23. Mhashamu Askofu Mathew Shija
24. Mhashamu Askofu Aloysius Balina
25. Mhashamu Askofu Norbert Mtega
26. Mhashamu Askofu Amedeus Msarikie
27. Mhashamu Askofu Patric Iteka
28. Mhashamu Askofu Emmanuel Mapunda
29. Mhashamu Askofu Telephor Mkude
30. Mhashamu Askofu Gabriel Mmole
31. Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa
32. Mhashamu Askofu Justine Samba
33. Mhashamu Askofu Fortunatus Lukanima
34. Mhashamu Askofu Paul Ruzoka
35. Mhashamu AskofuBruno Ngonyani
Rejea
[1]. Encyclicals; Rerum Novarum, May 15, 1891, Quadragesimo Anno, May 15, 1931; Mater et Magistra, May 15, 1961.
[2]. Solicitudo Rei Socialis, December 30, 1982 No.41; Populorum Progressio, March 26, 1967 No.12.
[3]. Gaudium et Spes No.11.
[4]. Waefeso 6: 14 - 16
[5]. Mwanzo 2: 26
[6]. Mwanzo 2: 7
[7]. Mwanzo 1: 28 - 31
[8]. Populo.rum Progressio No 34
[9]. Ufunuo 22: 13
[10]. Wakolosai 1: 15 - 20 na kuendelea
[11]. Ufunuo 21: 5
[12]. 1 Wakorintho 15: 54
[13]. 1 Wakorintho 15: 24
[14]. Solicitudo Rei Socialis No. 32
[15]. Solicitudo Rei Socialis No.-35
[16]. Solicitudo Rei Socialis No 36
[17]. Popularum Progressio No. 14
[18]. Zaburi 127.1
[19]. Zaburi 128: 1 - 2; 4
[20]. Centesimus Annus No. 6
[21]. Mwanzo 3: 19
[22]. Mwanzo 1: 28
[23]. Populo,rum Progressio No. 22
[24]. Populo.rum Progressio No. 22
[25]. Centesimus Annus No. 50 - 51
[26]. Centesimus Annus No. 37
[27]. Mwanzo 1: 26 - 28; 2: 7
[28]. Waefeso 3: 15
[29]. Humanae Vitae No 2 na Populorum Progressio No 37
[30]. Mwanzo 2 : 7
[31]. Isaya 42: 5
[32]. Matendo 17: 24 - 25
[33]. Kumbukumbu la Torati 32: 39
[34]. 1 Samwel 2.6
[35]. -KUmbukumbu la Torati 5 : 17
[36]. Mwanzo 1: 27 – 28
[37]. Zaburi 127: 3 – 5
[38]. Zakaria 8: 4 - 5
[39]. Humane Vitae No 7 - 17
[40]. 1 Yohane 4.8
[41]. Waefeso 3: 15
[42]. Gaudium et Spes No. 511
[43]. Humanae Vitae No 4 na 18; Gaudium et Spes No 48 na Lumen Gentium No. 35
[44]. Humanae Vitae No 10 - 13 na Lumen Gentum No. 35 na Gaudium et Spes No. 48
[45]. Solicitudo Rei Socialis No 29; Populorum Progressio No. 34
[46]. Mathayo 4.4
[47]. Centesimus Annus No. 46
[48]. Centesimus Annus No. 46
[49]. Centesimus Annus No. 46
[50]. Solicitudo Rei Socialis No. 15
[51]. Mathayo 5: 16
[52]. Mathayo 9: 37 - 38