Text Size

Tume ya Haki na Amani

Tume ya Haki na Amani

 Barua Ya Kitume Ya Maaskofu Wakatoliki Wa Kenya

 1 January 1988

 


The subject matter of this Pastoral Letter is the establishment of a Catholic Justice and Peace Commission at the national level under the responsibility of the Kenya Episcopal Conference. The motivations to establish such a Commission were of different kinds. First of all, the example of Pope Paul VI, who, in the wake of the Second Vatican Council, decided by his Motu Proprio, Catholicam Christi Ecclesiam (6 January 1967), to establish the Pontifical Commission Iustitia et Pax. This gave an example of promotoing justice and peace and provided inspiration and support for each local church to establish a similar body in its own social and cultural context, as the Pope intended, according to his Encyclical Letter On Progresss of the Peoples, (1967) No. 5.

 

 The Symposium of Episcopal Conferences of Africa and Madagascar (SECAM), founded in Kampala in 1969, followed this same line. At its plenary meeting in Nairobi (1978) the central theme was precisely "Justice and Peace in Africa." The representatives insisted on the need to promote justce and peace. In its plenary meeting of 1981, in Yaounde, the central theme was "Justice and Evangelization in Africa." The Bishops were explicit in inviting all the Bishops' Conferences in Africa to establish Justice and Peace Commissions at the National level. (See SECAM, Justice and Evangelization in Africa, Yaounde - Cameroon, 1981, No. 31).

The Bishops of Kenya appointed, in 1984, an "ad hoc" Committee to study the way the Catholic Justice and Peace Commission should be established and structured. The draft of this Pastoral Letter, after consultation with several difference groups, was carefully studied and amended by the Bishops themselves. This explains why it was ready only four years later, in January 1988.

 The social context of Kenya also motivated the Bishops. They realised that injustice was growing, due to both external and internal causes. The gap between the small number of the rich and the great number of the poor was increasing. Political tension since the establishment of the one-party State and the "queuing system" of voting were also matters of concern implicit in this Letter.

 Utangulizi

 1. Mungu aliwaumba Wanadamu kwa mfano wa sura yake Mwenyewe. Akawaita washiriki hali ya maisha yenye furaha na ya Umoja na Yeye Mwenyewe. maisha ambayo yangeanza hapa duniani na kufikia ukamilifu wake huko mbinguni. Aliwakabidhi jukumu la kuitunza dunia, kuisitawisha na kuitumia kwa utaratibu ambao kwake, ungewezesha watoto wote wa Mungu kushirikishwa kwa usawa katika furaha yake. (Mwanzo 1:26-27).

 2. Lakini mpango wa Mungu kwa ulimwengu wake, ulikumbwa na upinzani, wakati binadamu alipochagua kufuata ushawishi wa shetani, akageuka adui wa Mungu, na kuanza kutafuta utimilifu katika viumbe badala ya Muumba Mwenyewe.

 Ugomvi, taabu na mashaka, zilichukua pahali pa utangamano, uzuri na kupendana.

 

 Kile ambacho kingalikua na kuenea na kuonyesha zaidi na zaidi utimilifu wa Mungu Mwenyewe, kiliharibiwa, na uovu ukaingia ulimwenguni. (Mwanzo 3.4-5)

 

 3. Yesu Kristu, Mwana wa Mungu Mwenyewe, alifanyika binadamu na akajitwika jukumu la kuturudisha katika urafiki wa Mungu, na kuleta tena utangamano, amani na upendo katika ulimwengu. Alieleza utume wake kama ifuatavyo:

 

 "Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru walioteswa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa." Lk. 4:18-19)

 Yesu aliamuru Kanisa lake kuendelea na kazi hii hata baada ya yeye kurudi kwa Baba, na akamtuma Roho Mtakatifu kulipatia Kanisa nguvu na uongozi katika utume wake.

 Utume wa Kanisa juu ya Haki na Amani

 4. Kanisa katika Kenya limeshirikiana katika utume huu wa ukombozi tangu siku zake za mwanzoni kabisa, likihubiri Habari Njema za kupatanishwa kwetu na Mungu, likitekeleza upatanisho huu kwa huduma zake za Sakramenti, na likijitahidi kuwafikishia binadamu wote ufalme wa Mungu

 "Ufalme wa ukweli na uzima, ufalme wa utakatifu na wa neema, ufalme wa haki, mapendo na amani."[1]

 5. Wakati wote Kanisa linafahamu kwamba, Mungu anataka ufalme huu uwe wa kweli na hakika sio tu katika maisha ya ulimwengu utakaokuja, lakini pia katika maisha haya haya ya humu duniani, kwani kulingana na vile Kristu alivyotuambia kwamba "Ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.... Ufalme wa Mungu umo ndani yenu" (Lk. 11:20; 17:21 ). Hii ndiyo sababu Kanisa wakati wote limejishughulisha kwa makini sana juu ya hali njema ya binadamu hapa duniani, pamoja na maisha ya milele mbinguni. Mahali watu walipokosa elimu, Kanisa lilianzisha shule, hata katika sehemu za mbali na ngumu kwa mawasiliano. Kanisa lilipeleka huduma za afya na hospitali kule zilikohitajika zaidi. Kanisa kila wakati lilikuwa tayari kutoa msaada wakati wa njaa na shida zingine, na kutekeleza mipango ya kuwafuliza wale waliopatikana na misiba na ukosefu wa mahitaji muhimu ya maisha.[2]

 "Maendeleo ya moja kwa moja ya jamii za watu ni jambo ambalo Kanisa linajishughulisha nalo kwa makini sana. Jambo hili huwa la kweli hasa kuhusiana na zile jamii za watu ambazo zinajaribu kuondokea maangamizi ya njaa, umaskini, magonjwa na ujinga; pia kwa zile jamii zinazotafuta kupata sehemu kubwa zaidi ya faida ya ustaarabu, na taratibu za kuendeleza vipawa vyao vya kibinadamu; pia kwa jamii zile, zikiwa na fahamu kamili zinajitahidi kukua hadi utimilifu zaidi. Kanisa likiwa na ufahamu ulio wazi zaidi tangu mtaguso mkuu wa Vatican ya Pili, juu ya maagizo yanayoamuriwa na Enjili ya Kristu kuhusu jambo hill la maendeleo ya jamii za watu, limeamua kwamba ni wajibu wake kuwasaidia binadamu wote kuchunguza tatizo hili zito katika hali zake zote, na kuwaaminisha umuhimu wa kuchukua hatua kwa pamoja wakati huu muhimu na wa hatari."

 Kanisa linaendelea kujipa sharti kutimiza utume huu lililopewa na Mungu, utume wa maendeleo ya binadamu, kuendeleza haki, mapendo na amani. Baba mtakatifu Paul VI alieleza jambo hili kinaganaga hivi:

 "Likifuata kwa ukweli mafundisho na mfano wa mwanzilishi wake Mwana wa Mungu, ambaye alitaja kuhubiri Enjili kwa maskini kama ishara ya utume wake, Kanisa halijakosa kusaidia maendeleo ya kibinadamu ya mataifa yote ambayo linayaletea imani katika Kristu."[3]

 Kanisa lakini linajikuta bado katika hali ambapo ukosefu wa haki ni jambo la kawaida mno, na ambalo linaonekana kuzidi kuwa wazi na ovu zaidi. Katika dunia yote, pengo kati ya mataifa tajiri na yale maskini bado linabaki, na pengo linazidi kupanuliwa na taratibu za biashara ya kimataita, mzigo wa madeni, na maongozi yenye uchoyo ya nchi nyingi tajiri na ya mashirika ya kitaifa.

 6. Pengo kati ya matajiri na maskini, kati ya wenye uwezo na wasio na uwezo, linaonekana katika nchi yetu. Udhalimu umeongezeka. Watu wachache wanamiliki utajiri na vinono vya nchi, huku watu wengi sana wakiwa hawawezi kujipatia mahitaji muhimu ya maisha. Ukosefu wa kazi na nyumba za kutosheleza, hali ya kutokuwa na usawa ya wanawake, kuvunjika kwa maisha ya familia kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, uvunjaji wa haki za kibinadamu kwa njia ya kuhamisha watu bila kuwapeleka mahakamani, ufisadi ulioenea sana na utumizi mbaya wa uwezo na madaraka katika mashirika ambayo yameundwa kuwatumikia wananchi, muhtasari wa kila siku magazetini yetu juu ya ukosefu wa uaminifu, dhuluma, wizi wa kutumia nguvu, hata mauaji - haya yote na maovu mengine mengi, yanazidi kuongezeka hivi kwamba, ule undugu wetu kama watoto wapendwa wa Baba mmoja, uko hatarini kusahauliwa na kupuuzwa. [4]

 ''Furaha na matumaini, Huzuni na uchungu wa binadamu wa wakati wetu, hasa wale amboa ni masikini au wanaumia kwa njia yoyote ile, ni furaha na matumaini, huzuni na uchungu wa wafuasi wa Kristu pia."

 Dai la Mungu Kwetu Sisi katika Kenya

 7. Hali hii ya ukosefu wa haki kuongezeka haipaswi kuachwa iendelee bila kuchunguzwa na kurekebishwa. Sisi ni wadeni wakubwa wa Mungu, kwa ajili ya baraka na vipawa vyake vyote katika maendeleo yetu kama taifa, hivi kwamba inatupasa kuwa waaminifu zaidi kwake.

 Kenya ni nchi ambayo ina uhuru na ustawi, iliyobarikiwa na amani na uthabiti wakati nchi nyingi zina vita na misukosuko, pia inaonyesha matumaini mema kwa siku zijazo, hivi kwamba, kufanikiwa kwake katika harakati zake nyingi, kunapasa kutushurutisha tuhakikishe kwamba, ule msingi wa wema, uadilifu na uchaji, ambao Kenya imejengwa juu yake unadumu imara na wenye nguvu. Ni kwa njia hii peke yake ambapo tunaweza kuonyesha kwa vitendo shukrani zetu kwa baraka za Mungu, na pia tuweze kuendelea kutumaini kwamba atakuwa pamoja nasi siku za usoni na wakati ujao.

 8. Kanisa linaitikia kwa furaha dai hilo likishirikiana na watu wote wa mapenzi mema, na lina hamu kutekeleza sehemu yake kufafanua maongozi ya jumuia yenye haki na furaha ambayo Mungu ametupatia, na ambayo imeelezwa vizuri sana kwenye mwito wa Rais wetu wa "Mapenzi, Amani na Umoja"[5] kwa sababu hii, maaskofu wa katoliki wa Kenya sasa wanaanzisha na kuweka Tume ya Haki na Amani, kama chombo cha Baraza la maaskofu. Kupitia chombo hiki wana matumaini kwamba, kanisa litaweza kutimiza kwa uzuri zaidi utume wa Kristu aliolipatia wa kukuza maendeleo yetu ya kibinadamu na ya Kiroho, na kuufanya Ufalme wa Mungu kuwa ukweli uliohai kati yetu.

 Madhumuni ya Tume Haki na Amani

 9. Madhumuni makubwa ya Tume hili ni haya:

 Kutengeneza na kutayarisha taratibu za mafunzo ya kuelimisha watu wawe na ufahamu zaidi wa mambo ya Haki. Taratibu hizi za mafunzo, kwanza zitaelekezwa kuwafanya watu binafsi wafahamu zaidi matakwa ya Haki katika maisha yao wenyewe, halafu zitaendelea a kuchunguza jinsi kanuni hizo za haki zinavyoweza kutekelezwa katika nia za watu na mashirika ya jumuia mbali mbali za nchi tunamoishi. Hatua ile ya kwanza, ni utangulizi wa lazima kabla ya hatua ya pili, kwa sababu bila juhudi kubwa ya kila mshiriki wa jumuia kutenda haki kwa mwingine, ni jambo lisilo la kutazamiwa kwamba kanuni za haki ya kijamaa katika jumuia zitaendelezwa.

 Kuongoza na kuunganisha kazi ya uchungaji ya kukuza haki na amani ndani ya Kanisa, na katika maisha ya kijamii, kiuchumi na kisiasa katika nchi yetu. Kwa kazi hii, mafundisho ya Kanisa kuhusu jamii ni lazima ipangwe yapatikane kwa namna rahisi, na katika lugha ambazo watu wataweza kuelewa kwa urahisi, na njia zote za mawasiliano ni lazima zitumiwe kuyajulisha mafundisho haya kwa njia inayofaa, ili yaweze kuwatia watu moyo wa kuchukua hatua za vitendo.

  • Kufanya kazi ili ukosefu wa haki ung’olewe kabisa mahali popote unapoonekana ukijiandaa, kwa mfano, katika swala la ugawanyanji wa ardhi, uvunjanji wa haki za kibinadamu, matendo yasiyo haki katika ukulima, Elimu, mambo ya afya, vyombo vya kupashiana habari, utalii nyumba na makao na kadhalika. Hapa ni lazima ikumbukwe kwamba hall ngumu za dhuluma na ukosefu wa haki, hazina matokeo au kuhusisha tu mambo ya kidini na kiroho, lakini zinaweza kuhusisha pia hali za asili ya ubinadamu, utamaduni na mila, kisheria, uchumi au siasa. Kwa sababu hii, italazimu mara nyingi tume hii kutafuta msaada wa wataalamu wa taaluma hizi ili mambo yachunguzwe vilivyo na suluhisho lipatikane.
  • Kuwapatia mashauri, kuwatia moyo na kuwapatia msaada wale wote wanaojihusisha na kuendeleza Haki na kupinga uvunjaji wa haki. Jambo hili hasa ni la lazima mahali panapowahusu maskini na watu wasio na uwezo au kujulikana. Mara nyingine watu huteseka kimya, au kwa sababu wanaogopa matokeo wakilalamika hadharani, au hawajui ni lipi wangefanya katika hali yao. kwenye visa kama hivyo, watu kama hawa inapasa wahakikishiwe msaada wa tume hii, na wapatiwe maelezo kuhusu taratibu zote na kadhalika, ili hali zao zirekebishwe na kuwa nzuri zaidi.
10. Katika kutimiza madhumuni haya, Kanisa ni lazima wakati wote liongozwe na roho ya mapendo na upatanisho, na ni lazima liwe mwangalifu kuona kwamba, Kanisa lenyewe litoe ushahidi wa kutenda haki katika maisha yake ya ndani na nje. Ili kuhifadhi kujitolea kwake kwa utendaji haki, Kanisa ni Lazima liwe na uangalifu sana wakati wa kukusanya habari sahihi kuhusu visa tofauti, ili lisiwe hatarini ya kuvunja haki, likishtaki wengine pasipo ukweli ati wamevunja haki.
Mwisho 
11. Kazi iliyo mikononi mwetu ni kubwa mno, hivi kwamba njia nzuri kabisa ya kuikabili, ni kushirikiana na mashirika na watu wengine wanaotetea haki za binadamu. Katika moyo wa kushirikiana na uelewano wa makanisa, tume (itakapokuwa ni lazima) itafanya kazi pamoja na wakristu wa madhehebu mengine na watu wote wa mapenzi mema. Wanachama wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Kenya, wanamuomba Mungu aibariki kazi hii waliojitwika, na pia tunawahimiza wafanyi kazi wanaohusika, kutimiza wajibu wao kwa ushujaa, busara na nia dhabiti. Tunawasihi wakritu wote, na watu wote wapendao amani wazingatie Haki na amani, ili nchi yetu ya Kenya izidi kwenda mbele na kufanikiwa.

Sisi, Tunawabariki na Kudumu,
Wenu Wampendao sana katika Kristu, 

Rt. Rev. Ndingi Mwana 'a Nzeki,
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, Askofu wa Nakuru
H.E. Maurice Cardinal Otunga,
Askofu Mkuu wa Nairobi
Rt. Rev. Silas S. Njiru,
Makamu wa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, Askofu wa Meru.
Rt. Rev. W. Dunne,
Askofu wa Kitui
Rt. Rev. T. Mugendi,
Askofu wa Kisii
Rt. Rev. J. Njenga,
Askofu wa Eldoret
Rt. Rev. P. Sulumeti ,
Askofu wa Kakamega
Rt. Rev. U. Kioko,
Askofu wa Machakos
Rt. Rev. C. Davies,
Askofu wa Ngong
Rt. Rev. J. Mahon ,
Askofu wa Lodwar
Rt. Rev. Z. Okoth,
Askofu wa Kisumu
Rt. Rev. N. Kirima,
Askofu wa Mombasa
Rt. Rev. A. Ravasi,
Askofu wa Marsabit
Rt. Rev. P. Kairo,
Askofu wa Murang'a
Rt. Rev. P. Darmanin ,
Askofu wa Garissa
Rt. Rev. J. Njue,
Askofu wa Embu
Rt. Rev. L. Atundo,
Askofu wa Bungoma
Msgr. Vaccari,
Jimbo la Nyeri

 Notes

 [1] Sikukuu ya B.W. Yesu Kristu Mfalme Prefatio ya Misa

 [2] Baba Mtakatifu Paul VI - Populorum Pregressio No. 1 (Maendeleo ya Jamii za Watu No. 1)

 [3]Populorum Progressio No. 12.

 [4]4. Maandiko ya Vatican II: Kanisa katika Dunia ya Kisasa No.1

 [5]Nyayo Philosophy

 Questions for Reflection and Sharing

 

 a. How had the Church been committed to justice and peace "from her earliest days" in Kenya (Cf. No. 4-5)? What new approach is then brought by a Justice and Peace Commission now?

 b. How would you describe the role of a Diocesan or Parish Justice and Peace Commission?

 c. How could Small Christian Communities be committed to the promotion of Justice and Peace?

 d.The Justice and Peace Commission has organised since 1988 a National Lenten Campaign every year. Have you actively participated in it? How do you evaluate it?